![]()  | 
| Mwanadada aliyetambulika kwa jina la Asha baada ya kufumaniwa akisindikizwa na ngoma. | 
Na Dustan Shekidele, Morogoro
AMA
 kweli dunia ina mambo na mambo yenyewe ndiyo haya! Katika hali ya 
kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ramadhan Ally, mkazi wa 
Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amewashangaza wengi kufuatia uamuzi
 wake wa kukodi ngoma ya asili kwa lengo la kwenda kumfumania mkewe 
aliyejulikana kwa jina moja la Asha.
Tukio
 hilo lililofunga mtaa lilijiri asubuhi ya saa 3:14  Jumatatu iliyopita 
eneo maarufu kwa jina la Sultani baada ya mwanaume huyo kutonywa kuwa, 
mke wake alikuwa amelala kwa rafiki yake kipenzi, Abdallah Elias.
Baadhi
 ya wananchi waliobahatika kuwasili katika eneo la tukio walishuhudia 
mwenye mali akiwashushia kichapo kikali ‘wasaliti’ hao ambapo vurugu 
zikapamba moto.
Kufuatia
 hali hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa huo waliamua kutoa taarifa kwa 
Kamanda Mkuu wa Ulinzi wa Jadi Kata ya Mbuyuni, Aidan Mtimbo ambaye 
alifika eneo la tukio na vijana wake na kuwasomba watuhumiwa hao 
msobemsobe huku wakisindikizwa na ngoma hiyo hadi Kituo cha Polisi Kata 
ya Mbuyuni.
Katika
 hali ya kushangza, nje ya kituo hicho cha polisi baadhi ya wananchi 
waliokuwa na hasira walishinikiza watuhumiwa watolewe nje wawafanyie 
kitumbaya huku baadhi yao wakikipopoa mawe kituo hicho kilichokuwa na 
askari mmoja aliyevaa nguo za kiraia.
Baada
 ya vurugu hizo, afande huyo alipiga simu kituo kikuu cha polisi kuomba 
msaada ambapo askari wa pikipiki walifika na kuwakodia teksi watuhumiwa 
hadi kituoni.
Mwandishi
 wetu alifanikiwa kuwahoji wahusika wote watatu ambapo mume wa mwanamke 
huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kama ifuatavyo:
“Huyu mwanamke ni malaya sana, kwanza  nimemtoa kwao Matombo (Morogoro) akiwa na watoto wawili na kila mmoja na baba yake.
“Mimi
 sikujali hilo, ukipenda bonga penda na ua lake. Miezi mitatu iliyopita 
aliniambia ana ujauzito wangu, taarifa hizo zilinifurahisha sana. Cha 
ajabu juzi akaniambia ametoa mimba yangu, nilipomuuliza kwa nini, 
akasema kwa ujeuri eti hayupo tayari kuzaa na mimi kwa sasa.
“Nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao, jana usiku napokea taarifa kuwa yuko nyumbani kwa rafiki yangu kipenzi, Abdallah Elias.
“Ndiyo asubuhi nikakodi ngoma na kwenda, niliwakuta wamelala kitandani.”
Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema: 
“Huyu
 mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, 
yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia  amefukuzwa na mumewe hivyo 
anaomba alale kwangu kesho  yaani leo aende kwao Matombo kumbe 
alisharudishwa kwao toka juzi.”
Naye mwanamke huyo alipohojiwa na paparazi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Huyu
 mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi 
wangu ananipiga danadana. Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa
 naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”
Diwani
 wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya amethibitisha kutokea kwa fumanizi 
hilo kwenye mtaa wake lakini aliwatupia lawama polisi wa pikipiki kwa 
kupuuza uongozi wa juu wa kata hiyo ambao kwa kushirikiana na walinzi wa
 jadi walifanikiwa kuwalinda watuhumiwa wao na kufika salama kwenye 
kituo cha polisi.
GPL

0 comments:
Post a Comment