May 29, 2014

  • TASWIRA MBALI MBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO



    TASWIRA MBALI MBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
    Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, bungeni mjini Dodoma Mei 29, 2014.
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu Maswali Bungeni mjini Dodoma Mei 29, 2014.
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wasanii kutoka kikundi cha Pilipili Entertainment, Ahmed Olotu maarufu kwa jina la Chillo (katikati) na Madame Kitu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 29, 2014.
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi (wapili kulia), Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (wanne kulia)na Waziri wa Uchukuzi,Dr. Harison Mwakyembe (wasita kulia) wakizungumza na Wananchi kutoka wilayani Hai ambao walikuja bungeni kuonana na Waziri Mkuu, ili kuzungumzia mgogoro wa eneo wanaloishi lililopo karibu na Uwanaj wa ndege wa KIA. Wananchi hao pamoja na Mbunge wao, Freeman Mbowe walifanya mazungumzo na Mawaziri William Lukuvi na Dr. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Waziri Mkuu.
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Mei 29, 2014. Kutoka kushoto ni Kutoka kushoto ni Greyson Mlanga, Robert Bundala,Sadiki Selemani, Omar Lubuva ns na Emmanuel Simon.
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) baada ya kuzungumza nao Bungeni mjini Dodoma Mei 29, 2014. Kutoka kushoto ni Omar Lubuva, Emmanuel Simon, Greyson Mlanga, Robert Bundala na Sadiki Selemani.
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Viongozi wa Chama cha Wasioona TAnzania (TLB) baada ya kuzungumza nao ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Mei 29, 2014. Kutoka kushoto ni Omar Lubuvu, emmanuel simon, Greyson Mlanga, Robert Bundala na Sadiki Selemani.
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi kutoka Aga Khan Development Network ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Mei 200, 2014. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu na Ofisi Mkuu wa Masuala ya Fedha, Al- Karim Haji na Amin Kurji amabye ni Mwakilishi Mkazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.