May 28, 2014

  • BOTI YAZAMA NA KUUA WATU WATANO ZIWA VICTORIA





    BOTI YAZAMA NA KUUA WATU WATANO ZIWA VICTORIA

    Watu watano wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria.Kamanda wa Polisi wa Mkoawa Kagera, George Mayungaalisema ajali hiyo ilitokea Mei 23 mwaka huu saa 8 usiku. Boti 
    ya Mv Kitoko II waliyokuwa wakisafiria kutoka Bugombe kupitia Kasenye kwenda Mganza wilayani Chato, ilizimika ghafla ikiwa katikati ya ziwa.Alisema boti hiyo inayomilikiwa na Mama Chacha aishiye Muganza , 
    ilikuwa na abiria hao watano,ambao wote walikufa maji. Maiti 
    aliyepatikana ni mfanyabiashara raia wa Rwanda, Jane Mlekatete (36) 
    ambaye mwili wake ulikutwa ukielea. Wengine waliozama ambao 
    hawajapatikana ni Chikola Filbert (22) mkazi wa Muganza, Mapinduzi 
    Daud ( 38 )mkazi wa Mwanza, Ashana Suzy waliotambuliwa kwa jina moja 
    moja, wote wakazi wa Kasenyi na Mavombe (23) ambaye ni mkazi wa 
    Muganza.Alisema chanzo cha ajali hiyo ni boti kubeba mzigo mkubwa. Kwa 
    mujibu wa Kamanda, ilikuwa imebeba magunia 210.Chanzo kingine cha 
    ajali hiyo ni kwamba licha ya kubeba mzigo mkubwa, ilisafiri usiku 
    wakati kukiwa na upepo mkali na mawimbi yaliyosababisha injini ya 
    botihiyo kuzimika kabla ya kuzama.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.