Tapeli Sugu aliyejulikana kwa Jina la Ally Mwinyi Kutoka Vikindu-Pwani aliyekamatwa Parking za Madereva wa Wabunge-Dodoma akiwa chini ya Ulinzi tayari kwa Kupelekwa Kituo cha Polisi kwa hatua za Kisheria.
Akificha
Uso wake asipigwe Picha na Mtambo wetu wa
Habari.
Akiwa
Chini ya Ulinzi Mkali.
Akipandishwa
kwenye Gari la Polisi kupelekwa Kituoni kwa hatua zaidi za
Kisheria.
Kijana
Mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mwinyi na Kujitambulisha anatokea
VIKINDU-Pwani amekamatwa na Jeshi la polisi kwa Ushirikiano na Madreva wa
Wabunge hapa Dodoma kwa tabia yake Mbaya ya Kutapeli
watu.
Kijana
huyo amekuwa akijihusisha na Matukio Mbalimbali ya Utapeli hapa Dodoma kwa
nyakati tofauti na kwanji tofauti na kwa watu tofauti.
Utapeli
wake amekua akiufanya kwenye Uuzaji wa Viwanja akijidai yeye ni Dalali wa
Viwanja,Pia amekamatwa akiwa na Fungo “FAKE” za Gari ambazo amekuwa akitumia
kutembea nazo na kujidai yeye ni Dreva wa TASAF amekwama Dodoma hivyo anahitaji
Msaada,Kwa nyakati tofauti Madreva wamekuwa wakikutana naye na kuwaomba masaada
na hatimaye Kupewa fedha za Kumuwezesha Kurudi Dsm alikosema ndio anafanya kazi
ya TASAF.
Lakini
hadi jana anakamatwa akiwa kwenye jaribio la Kumtapeli Dreva wa Mh:Makongoro
Mahanga, ameshadanganya Madreva Wengi na bado amekuwa akionekana Dodoma tofauti
na maelezo yake kuwa anahitaji msaada wa Nauli arejee Dsm tangu Bunge la Katiba
Kuanza,Pia ameshukiwa kutapeli watu wengi fedha likiwamo jaribio la Kuiba
pikipiki eneo la Kituo cha Polisi Dodoma.
Wakati anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Rai,Kama
Umetapeliwa Dodoma,tafadhali fika Kituo cha Polisi Dodoma Mjini kwa msaada
zaidi.
0 comments:
Post a Comment