May 27, 2014

  • KIBAKA akimbilia Kanisani Ubungo baada kunusurika Kifo kutoka kwa Wananchi…Aamua Kuokoka



    KIBAKA akimbilia Kanisani Ubungo baada kunusurika Kifo kutoka kwa Wananchi…Aamua Kuokoka
    Mtu mmoja ambaye alikuwa akishiriki vitendo vya wizi alijikuta akimpa Yesu maisha yake hapo jana mara baada ya kukimbilia kanisa la The Oasis Healing Ministries lililopo nyuma ya jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam, mara baada ya mwizi huyo kukimbilia kanisani hapo akisalimisha maisha yake baada ya kuiba alikotoka.
    Mwizi huyo ambaye hata hivyo GK haikupata jina lake, mara baada ya kukimbilia kanisani hapo, aliweza kuhubiriwa neno la Mungu ambalo alilipokea na kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na kuahidi kuendelea kumshika na kumkiri Yesu, hata kokote atakapopelekwa na jeshi la polisi ambao walifika kanisani hapo kumchukua mwizi huyo.
    Mwizi akifanyiwa maombi                  akiwa ndani ya gari la polisi
    Mwizi akifanyiwa maombi akiwa ndani ya gari la polisi

    Tukio la mwizi huyo kumpokea Yesu lilipokelewa kwa shangwe na waumini wa kanisa hilo ambao walishindwa kuzuia furaha hiyo hata mwizi huyo alipopandishwa kwenye gari ya polisi, ambapo mchungaji alimuombea huku mwizi huyo akionekana mwenye utulivu.

    Maombi yaliendelea, alipata                  neema ya ajabu kwakweli.
    Maombi yaliendelea, alipata neema ya ajabu kwakweli.
    Maisha yake amempa BWANA.
    Maisha yake amempa BWANA.
    Waumini wakifurahi tukio                  lililotukia
    Waumini wakifurahi tukio lililotukia
    Gari alilopakizwa mwizi                  huyo
    Gari alilopakizwa mwizi huyo


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.