May 27, 2014

  • PPF KANDA YA KINONDONI YANG’ARA KATIKA MAONESHO YA 2 YA KIBIASHARA YA TANGA

    Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni inayojumuisha wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Pwani (Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo) na mkoa wa Tanga Bi Zahra Kayugwa akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa PPF katika viwanja vya Tangamano. Mfuko wa Pensheni wa PPF unawakaribisha Wanachama na Wadau wote kutembelea katika banda lao ili kupata elimu kuhusu mafao na huduma mbali mbali zitolewazo na PPF.
    Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda akisikiliza kwa makini maelezo ya Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni inayojumuisha wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Pwani (Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo) na mkoa wa Tanga Bi Zahra Kayugwa wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 2 ya Kibiashara mkoani Tanga.
    Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni Bi Zahra Kayugwa akiwa katika picha pamoja na washiriki wengine wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 2 ya Kibiashara mkoani Tanga katika viwanja vya Tangamano.  
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.