HUU
ni msiba mwingine mkubwa, tene pengine ni msiba mkubwa zaidi. Producer,
Director na mwandishi wa filamu pamoja na tamthilia, George Tyson
amefariki kwa ajali ya gari.
Habari zilizoifikia Saluti5 zinasema Tyson alikuwa akitokea Dodoma kurejea Dar es Salaam na ndipo akapata ajali hiyo.
Tyson
ndiye mtu aliyeleta mapinduzi ya tahmthilia hapa nchini, lakini pia
akafanya mageuzi katika filamu kwa kuitoa kwenye kuuza sura hadi kuwa
biashara. Alishiriki katika kuandaa filamu ya Girlfriend iliyoleta
mapinduzi makubwa.
Habari zaidi zitakujia baadae.
0 comments:
Post a Comment