Na Nathaniel Limu, Ikungi
KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya
Shanta Mining Ltd imetoa leseni tatu na mtaji wa shilingi milioni 40 kwa kikundi
cha wachimbaji wadogo cha Aminika cha kijiji cha Mang’onyi Wilayani Ikungi,
Mkoani Singida.
Kikundi hicho Aminika Gold Mine Co- Operative
Society Ltd Mang’onyi, kimekabidhiwa leseni hizo hivi karibuni na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Stepheni Maselle kwenye kijiji cha Sambaru.
Akikabidhi leseni hizo Naibu Waziri Maselle
amewataka wanakikundi kujipanga vizuri katika kuanza kufanya kazi ya uchimbaji
dhahabu ili kujikwamua kimaendeleo.
Aidha amesema ni matarajio yake kuona kuwa
kikundi hicho kinakuwa na maendeleo na kuwa mfano wa kuigwa hapa nchini kwani
tayari nguvu kazi wamepewa mtaji na Shanta.
“Ndugu zangu sijui Mungu awape nini mmepewa
leseni, mmepewa mtaji na vifaa vya kuanzia kazi na hawa wenzetu wa Tan Discovery
mnaoneshwa eneo ambalo tayari limefanyiwa utafiti, sasa kazi kwenu.” Amesema
Maselle huku akishangiliwa na wananchi.
Aidha aliwataka wanakikundi hao kutumia kama
SACCOS katika kukopa sehemu mbalimbali za kifedha kwa manufaa yetu na kizazi cha
baadae.
Hata hivyo Naibu Waziri, Maselle amesema ni
dhamira ya serikali kuendeleza wachimbaji wadogo hapa nchini kwa kuwapatia
mafunzo na namna bora ya uchimbaji
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Steven Maselle akimkabidhi Katibu wa Kikundi cha Aminika Ltd cha kijiji cha
Mang’onyi Wilayani Ikungi, Hamis Kingi,moja ya leseni tatu za uchimbaji wa
madini ya dhahabu zilizotolewa na Kampuni ya Shanta Mining Ltd, katika hafla
fupi za makabidhiano iliyofanyika Kijiji cha
Sambaru.
madini.
Katika risala ya wanakikundi cha Aminika
iliyosomwa na Katibu wake, Hamis Kingi amesema kikundi hicho ni muungano wa
vikundi vitano kutoka vijiji vitatu vitakavyoathirika na Mgodi wa Kampuni ya
Shanta Mining vyenye jumla ya wanachama 218.
Kingi alivitaja vikundi hivyo kuwa ni Elimika
Sambaru,Amani Sambaru, Amka Sambaru, Aminifu Mang’onyi na Muungano Mlumbi
ambavyo kwa pamoja vimeungana na kuwa kikundi kimoja kinachojulikana kwa jina
la Aminika
Aidha alitanabaisha kwamba vikundi baada ya
maelekezo hayo ya Serikali wachimbaji waliendelea kujiunga pamoja na kuunda
kikundi kilichofuata utaratibu wa kisheria wa kusajiliwa na kupata usajili
namba, SIR624 Kikundi cha Aminika Gold Mine Co – Operative Society Ltd –
Mang’onyi hatimaye wamekabidhiwa rasmi na Serikali.
“Mh,Naibu Waziri wa Nishati na Madini kwa kuwa
kikundi kiko Kisheria tunaomba Serikali kupitia Wizara yako ya Nishati na Madini
Makubaliano yetu kati ya Kampuni na Kikundi cha Aminika yaweze kutekelezeka kwa
muda mwafaka, kwani wanakikundi wanahitaji kufanya kazi ili kujikwamua
kiuchumi.”Alifafanua Kingi.
Naibu Waziri wa Nishati na madini
Steven Maselle akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samabru Wilaya ya Ikungi
Mkoa wa Singida wakati wa makabidhiano ya leseni tatu kwa wanakikundi cha
Aminika Ltd juzi.Picha na Nathaniel Limu.
“Pia tunakushukuru wewe binafsi kwa juhudi
zako kubwa kuwatetea wachimbaji wadogo kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini.”
Amesema.
0 comments:
Post a Comment