May 18, 2014

  • REAL MADRID YAANZISHA MBIO ZA KUMSAKA SUAREZ, BARCELONA NAO WAMO … dau lake nono kuilegeza Liverpool

     

    Spain-bound? Luis Suarez could spark a £100million bidding war between Barcelona and Real Madrid

    REAL MADRID inajiandaa kuanzisha mbinu zake za kawaida kwenye usajili kwa kupenyeza chokochoko kwa Liverpool na Luis Suarez.

    Madrid ambao wamekosa ubingwa wa La Liga lakini watakabiliana na Atletico Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa, wamepenyeza salam zisizo rasmi kwa mshambuliaji huyo wa Liverpool kwa kuwambia "Njoo ujiunge nasi".

    Gazeti moja la michezo la kila siku nchini Hispania limekuwa ndio chombo kikuu cha fitna za Real Madrid. Lakini imebainika kuwa timu hiyo haitakuwa na kazi ya kuishawishi Liverpool peke yake bali pia itakuwa inapambana na Barcelona ambayo nayo imeonyesha nia ya kuwania sahihi ya nyota huyo aliyetwaa tuzo tatu za England msimu huu.

    Hii inamaanisha kuwa thamani ya mchezaji huyo itapanda hadi pauni milioni 100. Katika kiwango hicho cha pesa, Liverpool itawawia vigumu kugoma kumpiga bei Suarez.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.