KIUNGO wa Hispania Cesc Fabregas amemkaanga Arsene Wenger kwa kufichua kuwa alifanya maongezi na kocha wa Arsenal kabla hajaamua kujiunga na Chelsea lakini akaambiwa nafasi yake tayari imezibwa na Mesut Ozil.
Arsenal walikuwa na nafasi ya kwanza ya kumsajili upya mara baada ya mchezaji wao huyo wa zamani kuamua kuondoka Barcelona, lakini hatimaye Fabregas akaamumua kujiunga na Chelsea kwa ada ya pauni milioni 30.
Mashabiki wengi wa Arsenal walicharuka mara baada ya Fabregas kusajiliwa Chelsea ambapo walitumia mitandao ya kijamii kushinikiza kocha huyo atimuliwe kwa kupuuzia kumrejesha kikosini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.
"Niliongea na Wenger lakini akaniambia itamuwia vigumu kunipatia nafasi uwanjani kwa vile Ozil ameziba vema nafasi yangu," alisema Fabregas katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye kambi yao ya Kombe la Dunia.
"Kulikuwa na sehemu nyingi za kwenda na nkaamua kuchagua klabu mbili au tatu zilizo bora, aliongeza kiungo huyo.
"Nikaongea na Jose Mourinho na akasema angependa kuwa nami. Kutoka hapo kila kitu kikaenda kwa haraka."
0 comments:
Post a Comment