Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka Kanda ya Ziwa wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam jana kwaajili ya Kuingia kambini tayari kwa safari ya kushindania Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane
Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kanda ya Nyanda za Kusini, Stephen Mapunda(mwenye kofia nyekundu) na Mtawa Kaparata (mwenye fimbo) wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere jana tayari kwa safari ya kushindania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Washindi wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakibadilishana Mawazo wakati walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam jana.
Washindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakielekea kwenye basi la TMT tayari kwa kupelekwa kwenye Hoteli kwaajili ya Kupumzika mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam. Picha zote na Josephat Lukaza.
Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka kanda zote za Tanzania wamewasili jijini Dar Es Salaam jana kwaajili ya kuingia kambini tayari kwa Kuanza safari ya kushindania kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la TMT itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Fainali hiyo ya aina yake inayotarajiwa kutoa Mshindi mmoja mkubwa ambae ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 ambapo washindi wengine tisa wakiungana na mshindi mmoja watacheza filamu ya pamoja ambayo itauzwa na kusambazwa na Kampuni ya Proin Promotions na washiriki hao kuweza kunufaika na Mauzo ya filamu hiyo.
Mara baada ya washindi 20 kutoka kanda zote sita wataingia Kambini mara baada ya kutoka kupima afya zao na hatimaye mchakato wa kumpata mshindi mmoja wa Shilingi Milioni 50 kuanza. Katika hatua hii ya kuanza kumtafuta mshindi wa milioni 50, Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) watakuwa wamepunguziwa majukumu kwa asilimia 40 na kazi hiyo kuelekea kwa wananchi ambapo watawapigia kura washiriki ambao wanawaona Wana vipaji na uwezo wa kuigiza.
Zoezi hilo la Upigaji kura litaanza mara moja mara baada ya washindi hao kuingia rasmi kambini na kuanza kupewa shule ya Sanaa na Walimu kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo.
Wananchi watawapigia Kura kwa Kutuma Ujumbe Mfupi wa Maneno.
chanzo:jiachie.
0 comments:
Post a Comment