May 18, 2014

  • Majangazz Kijana Afia kaburini wakati akijaribu kufukua maiti

     
     
     
     
    Maiti ya kijana huyo ikiwa imenasa kaburini
    ukio la ajabu na la kushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya kijana mmoja kukutwa akiwa amekufa kaburini,kijana huyo alikumbwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina.

    Kwa mujibu wa mtandao wa Saturday Tribune wa Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi walikimbia na kumuacha akihangaika kujinasua,lakini jitihada zake ziligonga mwamba mpaka pale umauti ulipo mkuta.
    "Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hilo waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka nae." Alisema mkazi wa eneo hilo.Soma zaidi hapa >>>>>

     
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.