June 16, 2014

  • BREAKING NYUZZZZZ.....: MICHAEL WAMBURA AONDOLEWA TENA UCHAGUZI MKUU SIMBA





    BREAKING NYUZZZZZ.....: MICHAEL WAMBURA AONDOLEWA TENA UCHAGUZI MKUU SIMBA
     Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba SC,Wakili Damas Ndumbaro akitoa tamko la kumuondoa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Simba SC,Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti,Michael Richard Wambura kwa kosa la kufanya kampeni kinyume na kanuni na sheria za Uchaguzi za TFF.Ndumbaro ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo amesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya Kamati yake kukaa na kujadiliana mambo mbali mbali kuhusu Uchaguzi huo Mkuu uliopangwa kufanyika Juni 29,2014,na kubaini kosa alilolifanya Wambura la kuanza kampeni mara baada ya kurudishwa kwenye kinyang'anyiro hicho.Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba SC,Issa Batenga.
     Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba SC,Bw. Amin Bakhresa akijibu moja ya mashwali yaliyoulizwa na waandishi wa habari juu ya uamuzi wa Kamati kumuondoa kwenye Uchaguzi Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti,Michael Wambura.
     Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini Mkutano huo,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam leo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.