Habari zimeenea nchini Afrika kusini kwamba Mwanariadha maarufu wa kike nchini humo Caster Semenya amejipatia mchumba wa kike.
Taarifa
katika vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa mahari au lobola kama
inavyojulikana Afrika kusini imepelekwa kwa familia ya mchumba huyo iliyoko
Polokwane jimbo la Limpopo na zikakubaliwa kwa mikono miwili na wazazi wa Violet
Raseboya.
Aidha
Lobola yaani mahari ya rand elfu 25 sawa na dola 2500 za Marekani ilikubaliwa
kwa mikono miwili.
Hata
hivyo Semenya mwenyewe anavilaumu vyombo vya habari kwa kuingilia maisha yake ya
kibinafsi .
Mwandishi
wa idhaa ya Kiswahili ya BBC nchini Afrika Kusini alipomtaka kuthibitisha kama
taarifa hizo ni za ukweli, Semenya alisema hatapinga au kukubali
Vyombo
vya habari nchini A-Kusini tayari vimeripoti kuwa Caster Semenya (23 ) amekua na
uhusiano wa kimapenzi kwa muda sasa na mwanariadha mwenzie wa kike Violet
Raseboya.
"Kama unanijua vizuri basi unafahamu
kuwa Caster hatangamani na vyombo vya habari. Nakutana na waandishi wa habari
wakati wa mashindano tu! Na wala sitajishugulisha kujibu kama madai hayo ni
kweli au la maanake ni swala ambalo limechapishwa magazetini siwezi kubadili
lolote!"
Mwanariadha
huyo aliyegonga vichwa vya habari kote duniani mwaka wa 2009 alipompiku Janeth
Jepkosgey wa Kenya na kutwaa ubingwa wa dunia wa mbio za mita 800 za wanawake
huko Berlin .
Wakenya
walikata rufaa wakitilia shaka jinsia yake kutokana na maumbile yake yenye
miraba minne.
Na
matukio yaliyofwatia yalimlazimu Semenya kufanyiwa uchunguzi wa siha na jinsia
na shirikisho la riadha duniani IAAF jambo lililompa fedheha sana bingwa huyo wa
dunia.
Aliporejea
nyumbani viongozi walioshabikia ushindi wake walimsifu kuwa binti wa Afrika
Kusini na hata magazeti ya urembo yakachapisha picha zake akiwa amejipodoa
.
Mwaka
wa 2006 wakati wa utawala wa Thabo Mbeki serikali ya Afrika Kusini ilipitisha
sheria ya kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja .
CHANZO:BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment