May 18, 2014

  • ROBBIE FOWLER AMLIPUA VAN GAAL …ASEMA HAIFAI MAN UNITED, NI MZEE …ataka Giggs apewe timu

     

    Help the aged: Robbie Fowler believes that Louis van Gaal is too old to manage Manchester United

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool, Robbie Fowler amehoji iwapo Louis van Gaal ni mtu sahihi kuinoa Manchester United, akiamini kuwa kocha huyo ni 'mzee' kwa kazi hiyo.

    Robbie Fowler ambaye katika enzi zake aliifungia Liverpool magoli sita dhidi United, anaamini Ryan Giggs angestahili kukabidhiwa timu.

    Tayari inaonekana Van Gaal atamchukua Giggs aliyepewa ukocha wa muda katika mechi nne za mwisho, kama msaidizi  wake.

    Lakini Fowler akasema katika maongezi yake na Alan Brazil Sports Breakfast show: "Sijui kama Van Gaal ni mtu sahihi kwa United. "Huwezi kubisha kuhusu ubora wake na mafanikio yake, lakini Manchester United inahitaji kocha kijana, kocha mahiri.

    "Wanapaswa kumpa Giggs. Ni moja ya nafasi kubwa sana katika soka, lakini Giggs anaijua klabu, anajua kinachotegemewa na afahamu  kila kitu kuhusu timu.

    "Siongei kama shabiki wa Liverpool kama mnavyofikiri. Nataka makocha vijana Uingereza wafanye vizuri kwasababu ni faida kwa soka la Uingereza kwa ujumla wake."

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.