May 18, 2014

  • MANCHESTER UNITED YAFANYA USAJILI WA KWANZA, YAMNYAKUA KIPA WA MIAKA 17 …aandaliwa kuwa mshindani wa kweli wa De Gea

     
     
     
     

    Signed: Man Utd have acquired 17-year-old Serbian goalkeeper Vanja Milinkovic

    MANCHESTER United imefikia maafikiano na FK Vojvodina kumsani kipa wa Serbia, Vanja Milinkovic kinda wa miaka 17.

    Hata hivyo kipa huyo ataendelea kubakia FK Vojvodina msimu ujao kabla ya kutua Old Trafford kuchuana na kipa namba moja David de Gea.

    Hakuna shaka juu ya ubora wa De Gea, ameonyesha kiwango cha juu msimu huu na kushinda tuzo mbili za klabu, lakini ujio wa Vanja Milinkovic utaongeza chachu ya ushindani kwenye lango la United.

    Milinkovic ni mchezaji tegemeo wa timu ya taifa ya vijana Serbia chini ya miaka 17, amecheza mechi sita katika kampeni za sasa za kufuzu UEFA Championship.

    Usajili wake unakuwa ni wa kwanza kwa mabingwa wa England mara 20, tangu walipomtimua kocha David Moyes mapema mwezi uliopita.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.