May 12, 2014

  • MTITU WA BONGO MOVIE ANG'ANG'ANIWA NA WANAWAKE BAADA YA KUVAMIA...!

     

     Muigizaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu.
    MUIGIZAJI na Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu amewashangaza watu baada ya kuibuka katika sherehe ya wanawake maarufu kama kibao kata cha Vanita Omary.
     Ishu hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa PG, Kinondoni jijini Dar ambapo mke wa staa huyo alikuwa miongoni mwa waalikwa lakini cha kushangaza Mtitu aliamua kumuibukia hadi ukumbini.

     "Mh! Hii kali ona sasa wanawake wameanza kumg'ang'ania bora angemsubiri nje," alisikika mwanamke mmoja lakini Mtitu hakujali, akamchukua mkewe, wakaondoka kwani sherehe ilikuwa imeshaisha.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.