June 01, 2014

  • Manchester United Yammendea Kiungo wa Real Madrid Kwa Dau La £25m





    Manchester United Yammendea Kiungo wa Real Madrid Kwa Dau La £25m
    Klabu ya Manchester United ipo tayari kutoa kiasi cha £25million kwaajili ya kumsajili Angel Di Maria baada ya winga huyo kukiri anaweza kuiacha Real Madrid.

    Kwa mujibu wa mtandao wa Merto Sport, maafisa wa Old Trafford wamemuweka Di Maria kuwa miongoni mwa wachezaji wa juu kwenye orodha ya majina ya wachezaji ambayo wanayafanyia kazi. Pia kwa mujibu wa ripoti za Hispania, United wapo tayari kutoa £25million na zaidi ili Di Maria aweze kutua Old Trafford.

    Di Maria, ambaye alifunga mabao 11 na kuisaidia Real Madrid msimu uliopita amesema ana furaha kuendelea kuichezea Real Madri na pia anaweza kuiacha klabu hiyo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.