May 08, 2014

  • Chama cha kilaghai kilichopata usajili kwa mara ya pili baada ya kufeli mpango ovu.




    Juzi chama kinachojipembua kuwa ni chama cha siasa cha ACT kimepata
    usajiri wa kudumu,

    Mazingira ya upataji usajili wa kudumu yamejaa utata mtupu na ni
    hatari kwa demokrasia ikiwa mamlaka za nchi zinaruhusi makundi haya ya
    kihuni kuitwa chama cha siasa na kupewa usajili.

    Nitaeleza kwa kifupi ujio wa kinachoitwa chama na kilikotokea na madhumuni yake.

    Mwenyekiti wa ACT ni Kadawi Limbu, Na huyu huyu Kadawi Limbu ndiye
    Mwenyekiti wa ADC (kipindi inaanza na haijulikani ni lini alihama) .
    Na akiwa ziara sometimes anaenda Kama Mwenyekiti wa ADC na sometimes
    anaenda Kama Mwenyekiti wa ACT hii wengi hawajaigundua huyu jamaa
    anavyofanya

    Na pia, huyu Kadawi Limbu ni mdogo wake na Festus Limbu Mbunge wa
    Jimbo la Magu kwa CCM, na kwao na huyu Kadawi Limbu ni Magu na Kwao na
    Mwigamba ni Magu Pia( do you see this connection).

    Sasa angalia matukio ambayo Kadawi ametumika ndani ya ACT na wakati
    huo huo ametumika ndani ya ADC

    http://issamichuzi.blogspot.com/2014/03/katibu-mkuu-wa-adc-katika-ziara-mkoani.html?m=1

    Fungua hiyo ni march 04, mwaka huu, akiwa na ADC

    Ya ACT angalia Mwenyekiti ni nani utakuta ni huyo huyo, kijana
    alicheza na nafasi ya Katibu wa ADC, na Mwenyekiti wa ACT kwa wakati
    mmoja, na Msajili wa vyama yupo kimya tu na hata wananchi wanaojiunga
    pia wengi hawajui hili, Hii inamaana ni UTAPELI na Ulagjai unaoendelea
    hapo.

    Na kuanzia hapa ni wazi kuwa wale waliofukuzwa Chadema mwaka jana they
    deserve kuwa nje ya CDM maana Kama ADC ni Ndugu wa ACT na ACT Mwigamba
    yupo na nafasi kubwa tu (nahisi ni Katibu mkuu ama Katibu Mkoa wa
    Mwanza), na ADC ilikuwepo hata kabla hawajapigwa chini na CDM hii ni
    wazi kuwa mission yao ilikuwa ni kuiua CDM.

    Na pia kuna uhusiano wa moja kwa moja Kati ya Kadawi Limbu na Hamadi
    Rashidi maana hawa wote ni waasi wa CUF, Kadawi kipindi flani
    aligombea ubunge moja ya majimbo Dar kwa CUF na Mara Hamadi alipotoka
    CuF naye akameguka ili kuwa mlezi wa ADC

    Kama mwezi juzi tu alikuwa anapiga ziara kama Katibu wa ADC, at the
    same time ana serve Kama Mwenyekiti wa ACT, kuna sheria inayoruhusu
    mtu mmoja kutumikia vyama viwili? ( Msajiri hapa alichemka), na hiyo
    connection ya Hicho chama strategies zao kubwa ni Lake zone, na wengi
    wa wafuasi wa Zito Kama Chagulani ( diwani wa Igoma) alikwenda jimbo
    la Nkenge ( kagera) na kuweka bendera za ADC kila Kona

    http://www.mpekuzihuru.com/2014/03/viongozi-wa-chama-cha-act-tanzania.html?m=1

    Hii link ya pili ni gazeti la March 17, mwaka 2014, tofauti ya wiki
    takribani 2 tu, mtu moja, sehemu moja ambayo ni Mwanza mjini, vyama
    tofauti.

    Haya ndugu zangu hizo ndio siasa za malengo ya mtawala
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.