June 13, 2014

  • KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA MAGEREZA MSTAAFU JOSEPHAT MWINGIRA AZIKWA



    KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA MAGEREZA MSTAAFU JOSEPHAT MWINGIRA AZIKWA
    Na Insp. Deodatus Kazinja,PHQ
    Aliyewahi kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Mzee Josephat Mwingira aliyefariki tarehe 09 Juni, 2014 na kuzikwa tarehe 12 Juni,2014 katika Makaburi ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam kwa heshima zote za kijeshi.
    Marehemu Mwingira aliajiriwa katika Jeshi la Magereza tarehe 11 January 1956 ambapo alianzia kazi katika Gereza Kuu Butimba la Jijini Mwanza na maeneo mengine mengi nchini hadi alipo staafu kwa mujibu wa sheria tarehe 01 Julai, 1990 akiwa amelitumikia Jeshi la Magereza kwa miaka 33.
    Hayati Mwingira mbali na kuwa kiongozi katika Jeshi la Magereza lakini pia alikuwa kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alishika nyadhifa kadhaa enzi za siasa majeshi.
    Kamishana Jenerali wa Jeshi la Magereza kwa niaba ya watumishi wote wa Jeshi la Magereza anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito.
    PIX 1Marehemu Josephat Mwingira

    PIX 2Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiingiza mwili wa Marehemu na kuuingiza nyumbani kwake baada ya kutoka "mortuary".
    PIX 3Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa aliyemwakilisha Kamishna Jenerali wa Magereza akitoa salaam za mwisho kwa marehemu.
    PIX 4Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mmeta Manyara (wa kwanza kushoto) akitoa heshma zake kwa marehemu
    PIX 5Baadhi ya wastaafu wa Jeshi la Magereza wakitoa salamu za mwisho kwa marehemu Mwingira (wa kwanza mbele) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Saimon Mwanguku, wa pili ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Alhaji Jumanne Mangara. Wawili hao walifanya kazi kwa karibu sana na Marehemu Mwingira enzi za uhai wake.
    PIX 6Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioko kazini na wastaafu kwa pamoja wakijumuika na wananchi wa kijiji cha Kilongawima Kata ya Kunduchi jijini Dar es salaam waliokusanyika na wanafamilia katika safari ya mwisho ya Marehemu Mwingira
    PIX 7Askari wa vyeo mbalimbali wakijumuika na wananchi wa kijiji cha Kilongawima Kata ya Kunduchi jijini Dar es salaam waliokusanyika na wanafamilia katika safari ya mwisho ya Marehemu Mwingira.
    PIX 8Mwenyekiti wa CUF Taifa na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kuli waliokaa kwenye viti) alikuwa miongoni mwa wananchi wa eneo la Kiliongawima Kata ya Kunduchi Jijini Dar es salaam katika kuifariji familia katika msiba huo mzito.
    PIX 9Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi (mwenye nguo nyeusi) alikuwa miongoni mwa wananchi wa eneo la Kiliongawima Kata ya Kunduchi Jijini Dar es salaam katika kuifariji familia katika msiba huo mzito. Marehemu Mwingira ni mzaliwa kijiji cha Mbaha Kata ya Lituhi Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
    PIX 10Mmoja wa ndugu za Marehemu Mwingira akitoa salaam za mwisho.
    PIX 11Msafara wa mwalimu wa Marehemu Mwingira kwenda katika makaburi ya Kunduchi Jijini Dar es salaam.
    PIX 12Ibada ya mwisho makaburini iliyoongozwa na Padre Paul Chiwangu kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania pamoja na Paroko wa Parokia ya Mtongani Padri Paul Malewa.
    PIX 13Baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza walioshirikia katika kuandaa na kufanikisha paredi la mazishi ya Marehemu Mwingira.
    PIX 14Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Mwingira wakiweka mashada ya maua.

    Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja, Makao Makuu ya Magereza


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.