Don't try It at home.
MZAHA SAINGINE WATAKA PLAN
Mdada mmoja alitaka kujua kiasi
gani
anapendwa na mume wake, hivyo
akataka kujua
mumewe atafanya nini endapo
ataamua
kuondoka na kumuacha!
Mwanamke huyo akaamua
kuandika barua
inayosema "Samahani mume
wangu, nimeamua
kuondoka na kwenda kuanza
maisha mapya
mbali na wewe"
Barua hiyo akaiweka juu ya meza
iliyokuwa
chumbani.
Baadaye jioni, muda wa Mumewe
kurudi
mwanamke huyo akajificha chini
ya uvungu wa
kitanda mule chumbani
Mume alipoingia chumbani
akakuta ile barua
juu ya meza, akaisoma kisha,
akaandika
maneno fulani kwenye ile ile
barua, harafu
akaanza kuimbaimba kwa furaha
huku akipiga
miluzi na akiwa anavua nguo.
Akapiga simu na akasikika akisema
hivi "hello
mpenzi, nina raha sana leo.. yule
mwanamke
nuksi amesalenda mwenyewe
kaondoka na
kutuachia uwanja, jiandae nakuja"
Muda huo huo Mume akaondoka.
Mwanamke alipokuwa uvunguni
akawa anatoka
lakini amenyong'onyea na
amelowa mashavu
kwa machozi.
Akasogea pale ilipo barua na
akataka kujua
mumewe aliandika kitu gani
kwenye ile barua.
Akakuta maneno haya "nimeona
miguu yako
uvunguni, tafadhali andaa chakula
nina njaa
sana mumeo, ila nimetoka kidogo
nafuata
maziwa nilisahau kupitia.
Nakupenda mke
wangu"
0 comments:
Post a Comment