June 21, 2014

  • BUNGENI JUNE 20 2014 GODBLESS LEMA AIVURUGA SERIKALI INAVYOONGEZA USHURU WA POMBE NA SIGARA

    June 20 2014 Mbunge wa Arusha mjini Kamanda Godbless Lema aliishambulia serikali ya CCM kwenye bunge la bajeti linaloendelea Dodoma kwa kusema…

    ‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’

    ‘Nimekwenda Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama chetu na Mh. Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida Same serikali imeweka vibao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA UPEPO MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali hauwekewi vibao vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’

    ‘Sehemu kubwa ya Singida na Dodoma ni semi desert, serikali ingeweza kabisa kutengeneza solar village maeneo haya ikatengeneza umeme mkubwa kupitia nguvu za jua ukaingizwa kwenye gridi ya taifa na mngeweza kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa huko mitaani’

    ‘Hata kama kutakua na mpango wa aina gani, unapokua na serikali ambayo haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema bado inakopesheka, bado tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi, ningekwenda kukopa barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli ijengwe, ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali yenu ihamie hapa Dodoma’

    ‘Watu wengi wamesema kuhusu serikali kuhamia hapa Dodoma, ukiondoa serikali Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa nguvu hii Ruaha ambayo hakuna watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu watu watakuwa wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya mapumziko itakua ni Iringa, Mbeya na Singida’

    ‘Mimi ningekua nyinyi ningefanya maamuzi magumu, ningechukua Mawaziri wote na makatibu wakuu wote waje hapa wakae gesti na wengine wakae kwenye matent kwa sababu msipochukua maamuzi serious hamuwezi kuibadili hii nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana kuzunguka kutafuta kura za Urais huko kote anakokwenda’

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.