May 10, 2014

  • BREAKIN NEWZZZ!!:- HATIMAYE MBEBEZ MUKHAREEZZZ KULIKO WOTE MBELEZZZ DMV/USA AWAFUNGA MIDOMO MAHASIDI WAKE AONYESHA BARUA ZA MUALIKO LIVE!!

     
     


    Missy Temeke Mkurugenzi wa KWETU Fashions hatimaye amefunguka kutokana na maoni ya watu waliopinga tangazo lake la kwamba amealikwa kwenye maonyesho ya tamaduni yanayofanywa na Balozi mbalimbali Washington, DC na kubeba jina la PASSPORT DC yakiwa chini ya Caltural Tourism DC na yanayoadhimishwa kila mwaka wakati huu wa majira ya spring.


    Missy Temeke akiongea na Vijimambo mchana leo Jumatatu May 5, 2014, amesema wanaosema sijaalikwa sio kweli muasisi wa PASSPORT DC alinifuata baada ya kuona meza yangu siku ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 50 ya Muungano na kuniomba barua pepe yangu na kwamba angependa niwe mmoja ya washiriki kwa kuiwakilisha Tanzania na pia kama naweza kuonyesha mitindo ya mbalimbali ya nguo za KWETU Fashions. Baada ya Hapo mawasiliano yalianza na mimi kuweka tangazo langu kwenye Vijimambo na waosha vinywa kuanza kusukutua bila mswaki huku wengi wakidai nadanganya na wengine kulazimisha kuleta vitu vyao bila kujua meza zimetolewa kwa hesabu.

    Mimi Barua yangu ya mwaliko hii hapa mchana kweupe na naomba aliyejileta kwa kudai maonesho yalikuwa ya wazi naomba nae alete barua yake ya mwaliko hapa Vijimambo.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.