May 25, 2014

  • UCHAGUZI SIMBA SC: KABURU, WAMBURA KITANZINI , NDUMBARO ASHIKILIA SHERIA MKONONI




    UCHAGUZI SIMBA SC: KABURU, WAMBURA KITANZINI , NDUMBARO ASHIKILIA SHERIA MKONONI
    http://ptblog.pesatimes.com/wp-content/uploads/2014/05/ndumbaro.jpg
    Dkt. Damas Daniel Ndumbaro
    KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Simba sc kesho inatarajia kuanza kusikiliza mapingamizi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Gymkan jijini Dar es salaam.
    Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwanasheria na wakala wa wachezaji wa FIFA, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amesema zoezi hilo litazingatia haki kwasababu kamati yake inajumuisha watu makini na wenye malengo ya kuipatia Simba sc viongozi bora.
    "Msimamo wetu uko pale pale, sisi hatumuondoa mgombea, bali kanuni za uchaguzi za TFF na katiba ya Simba ndio itamuondoa mgombea". Alisema Ndumbaro.
    Ndumbaro aliongeza kuwa wanasimba wawe na imani na kamati yake kwasababu haitapindisha sheria na kanuni hata kidogo.
    Aidha, Ndumbaro alisema watu wote waliowawekea pingamizi wagombea wanatakiwa kufika muda uliotajwa wakiwa na viambatanisho vyote hususani vithibitisho vya pingamizi zao.
    "Tulishawaandikia barua watu wote walioweka mapingamizi na kuwaeleza kila kitu. Lazima wawepo wakati wa kusikilizwa kwa mapingamizi yao kama sheria inavyotaka".
    "Kama mtu hatakuwepo, pingamizi lake halitasikilizwa" . Alisema Ndumbaro.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.