Mhe.Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mtoto Ridtwaik Lwal (13)aliyejeruhiwa mkononi kwa bomu
Mbunge wa viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM Mh.Catherine Magige amelaani vikali tukio la Bomu lililotokea katika mgahawa wa VAMA Tradition Indian Culture jijini Arusha huku akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo
Mh.Magige aliyasema hayo leo katika hospitali ya Selian wakati alipowatembelea majeruhi nane Raia wa Asia waliolazwa katika hospitali hiyo ambapo wengi wa majeruhi waliumia katika maeneo ya miguu,mikono na tumboni hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi kupoteza mguu wake wa kushoto
Magige alisema kuwa kutokana na matukio ya aina hiyo kutokea kwa mfululizo, hali hiyo imesababisha jiji la Arusha kupoteza amani ili hali Tanzania ni Nchi ya Amani'
"Inasikitisha sana kwa kweli matukio kama haya kujirudia rudia inatia hofu sana kwa wakazi wa Arusha pamoa na wageni wanaokuja katika jiji letu"alisema
Aidha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa vyombo vya dola kufanikisha kukamatwa kwa wale wote wanaohusika na matukio ya uvunjifu wa amani.(Pamela Mollel wa Jamii blog)
0 comments:
Post a Comment