ISHARA
za mwisho wa dunia? Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb amekula kichapo na
kuishia mikononi mwa polisi baada ya kunaswa katika nyumba ya kulala wageni
(gesti) akiwa na dogo wa kiume aliyedaiwa kuwa ni denti wa
sekondari.
Aibu hiyo ya karne ilijiri juzi Jumatatu kwenye gesti hiyo
(jina linahifadhiwa) iliyopo maeneo ya Manzese, Dar ambapo jamaa huyo alikutwa
chumbani na denti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14. Kwa mujibu wa
chanzo makini kilichoitonya Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global
Publishers, njemba huyo amekuwa na ‘katabia kachafu kakuwafanyia usodoma’ watoto
wa kiume.Habari hizo zilidai kuwa ishu hiyo iliwakera wakazi wa eneo hilo
waliokuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu ndipo wakaamua kumfungia kazi baada ya
kudaiwa kuwa na mtoto huyo chumbani usiku kucha. Kwa mujibu wa meneja wa
gesti hiyo (aligoma kuta jina) ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha kwa OFM,
raia hao walikuwa wakimchunguza njemba huyo kwa muda mrefu kutokana na tabia ya
kulala kwenye gesti hiyo na watoto wa kiume.
“Mwanzo tulifikiri anakuja
na vijana hao kama marafiki zake wa kawaida lakini tukaingiwa na wasiwasi baada
ya kugundua kuwa alikuwa akilala nao kwa kuwabadilisha,” alisema meneja
huyo. Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo
alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama
kawaida. “Wahudumu waliniambia kuwa jamaa amefika tena na amechukua chumba
cha juu lakini safari hii alifika peke yake, ilinishangaza sana kusikia kaja
peke yake kwani siyo kawaida yake so sikuamini,” alieleza meneja huyo. Alidai
kwamba asubuhi ya Jumatatu, mishale ya saa 4:00, wahudumu walisikia miguno ndani
ya chumba alicholala njemba huyo ndipo wakakifunga kwa nje kisha kuita polisi na
vijana wa OFM ambao walifika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’. Meneja
huyo alisema kuwa hafahamu njemba huyo alimuingiza kijana huyo muda gani kwani
walimuwekea mtego siku nyingi akawa anachezwa na machale. Hata hivyo, Jiji la
Dar huwa halina dogo kwani wakazi wa eneo hilo walijazana kwenye gesti hiyo
kutaka kumpiga jamaa huyo lakini polisi walifanikiwa kuwatorosha eneo hilo na
kuwampeleka Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar. Hadi OFM inang’oa nanga
kituoni hapo, njemba huyo na kijana aliyekutwa naye walikuwa wakiendelea
kuhojiwa
0 comments:
Post a Comment