May 17, 2014

  • Mwanafunzi wa Chuo kikuu wa SAUT jijini Mwanza auawa na wanafunzi wenzake kwa tuhuma za wizi

     


    Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini Mwanza, Helma Michael (22) ameuawa kwa kupigwa mawe na wanafunzi wenzake, wakimhisi kuwa ni mwizi wa kompyuta ndogo za mkononi na deki chuoni hapo.


    Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Valentino Mlowola, alisema juzi kuwa mwanafunzi huyo aliuawa Mei 13 mwaka huu saa 4.00 usiku, katika eneo la Nyamalango Malimbe, ambapo baada ya kubainika katika eneo hilo alianza kupigwa kwa mawe, fimbo na mapanga hadi kusababisha kifo chake: "Huyu ameuawa katika tuhuma ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa," alisema.
     
    Kutokana na mauaji hayo, watu 17 wamekamatwa na Polisi  imeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo huku Kamanda Mlowola akiwataka watu kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu ambao hawana hatia.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.