May 22, 2014

  • KIFO CHA KUAMBIANA, KOLETA AZIMIA, ALAZWA

     
     
     
     
    BAADA ya kupewa taarifa za msiba wa Adam Kuambiana, staa wa filamu za Kibongo, Coletha Rymond 'Koleta' alijikuta akizimia na kulazwa katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar. 
    Staa wa filamu za Kibongo, Coletha Rymond 'Koleta' akiwa hospitali baada ya kuzimia kwenye msiba wa msanii mwenzake Kuambiana.
    Sosi ambaye ni mtu wa karibu na staa huyo, alipenyeza habari kuwa Koleta alishindwa kustahimili taarifa hizo za msiba na kuzimia kwani alikuwa mtu wake wa karibu sana.
    Alipotafutwa na paparazi wetu mara baada ya kutoka hospitali juzi, Koleta alifunguka:
    "Kuambiana alikuwa mtu wangu sana, nilishindwa kabisa kuhimili kifo chake na kama unakumbuka ndiye ambaye nilianza kuigiza naye filamu yake ya kwanza ya Sauti ya Manka."
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.