Celi za Saratani ya Tezi Kibofu Huenda Saratani ya Tezi-Kibofu ni ugonjwa wa Zinaa unaosababishwa na ugonjwa wa zinaa ambao dalili zake sio wazi sana. Hii ni kwa mujibu wa wanasanyansi nchini Marekani. Wanasema kwamba Saratani hiyo husababishwa na maradhi fulani ambayo huenezwa wakati wa kitendo cha ngono. Lakini wataalamu wanasema kuwa ushahidi bado haupo kama kweli Saratani hiyo ni moja ya magonjwa ya zinaa na inasababishwa na magonjwa ya zinaa.
Ingawa baadhi ya
Saratani husababishwa na maradhi fulani fulani, kitengo cha utafiti wa Saratani
nchini Uingereza kinasema kuwa ni mapema mno kuongeza Saratani ya tezi kibofu
kwa Saratani hizo.
Wanasayansi
waliofanya utafiti huo walichunguza celi za tezi kifobu cha binadamu katika
maabara.
Waligundua kuwa
maradhi ya zinaa yaitwayo, 'Trichomoniasis' yalichochea ongezeko la Saratani
hiyo.
Hata hivyo mfumo wa
maisha pia unachangia ongezezeko la visa vya magonjwa ya Saratani.
Ugonjwa wa
'Trichomoniasis' unaaminika kuwaathiri watu milioni 275 duniani na moja ya
maradhi maarufu ya Zinaa ambayo hayasababishwi na Virusi
'Dalili za Trichomoniasis'
'Dalili za Trichomoniasis'
Kawaida, mtu hatapata
dalili za ugonjwa huo na inawezekana asijue kama anaugua ugonjwa
huo.
Wanaume huhisi
kujikuna sana ndani ya uume wao , kupata hisia za kuchomeka wakati wanapokwenda
haja ndogo au kuvuja majimaji meupe kutoka kwa uume wao.
Wanawake pia wana
hisia tu sawa na hizo katika sehemu zao za isiri pamoja na kuwa na harufu
mbaya.
Utafiti huu wa hivi
karibuni sio wa kwanza kuhusisha ugonjwa wa 'Trichomoniasis' na Saratani ya Tezi
kibofu.
Utafiti uliofanywa
mwaka 2009 ulipata kuwa robo ya wanaume walio na Saratani hio walikuwa na dalili
za ugonjwa wa Trichomoniasis na wanaume hawa pia walikuwa na uvimbe ambao
ulikuwa umekomaa mno.
'Hoja ya Uchunguzi zaidi'
Uchunguzi huo pia unaonyesha njiaambazo ugonjwa huo wa zinaa unawaweka wanaume katika hatari ya kupata Saratani ya tezi kibofu.
Profesa Patricia
Johnson na watafiti wenzake, waligundua kuwa viini vinavyosababisha ugonjwa wa
'Trichomonas vaginalis' - huvuja proteni ambayo husababisha Saratani ya Tezi
Kibofu kuzuka.
Mtaalamu wa afya,
Nicola Smith,anasema uchunguzi huu unaonyesha tu njia ambazo ugonjwa wa zinaa wa
Trichomonas vaginalis unazidisha uwezo wa mtu kuugua Saratani ya Tezi Kibofu na
kuchochea seli kukuwa kwa kasi.
"Lakini uchunguzi huu
ulifanywa tu katika maabara na matokeo ya awali kwa wagonjwa yalikosa kuonyesha
uhusiano kati ya ugonjwa huo na Saratani ya Tezi Kibofu,'' alisema Bi
Nicola
Kwa kauli hii
wanasema kuwa uchunguzi zaidi unahitajika ili kuabini hasa kinacho sababisha
Saratani ya Tezi kibofu kwani ugonjwa wa Trichomoniasis husababisha tu
mazinigira kwa ugonjwa huo kukomaa ila sio chanzo cha ugonjwa
wenyewe.
0 comments:
Post a Comment