August 19, 2014

  • Wazazi wana wajibu na ulazima wa kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora - Balozi Seif Ali Iddi



    Wazazi wana wajibu na ulazima wa kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora - Balozi Seif Ali Iddi
    Wazazi wana wajibu na ulazima wa kuhakikisha kwamba watoto wao wanawasimamia vyema katika kupata elimu bora itakayotoa mwanga wa kimaisha katika hatma yao ya baadaye. 

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akizunghumza na Uongozi wa Kamati ya Skuli, walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kinyasini Wilaya ya Kaskazini "A " mara baada ya kuikagua na kuangalia maendeleo na changamoto zinazoikabili skuli hiyo. 

    Balozi Seif alisema elimu ndio ufunguo pekee pekee utakaowapa njia watoto hao kukabiliana na mazingira ya kimaisha yanayokwenda kwa kasi na haraka ndani ya mfumo wa sasa wa sayansi na Teknolojia. 

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Kamati ya Uongozi ya Skuli hiyo kwa jitihada zake kubwa inazochukuwa kwa kushirikiana na walimu na kuleta maendeleo makubwa. Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee wa Skuli ya Sekondari ya Kinyasini Nd. Simba Haji alimuomba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufuatilia ahadi iliyotolewa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Mwisho wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutafuta mbinu za kulitengeneza Jengo la madarasa manne la Skuli ya Msingi ya Kinyasini ambalo liko katika hali mbaya. 

    Skuli ya Kinyasini ikiwa ni miongoni mwa skuli kongwe ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliasisiwa mnamo mwaka 1946 kwa Darasa la Quran na kuanza kwa darasa la kwanza mwaka 1947 lililoendelea hadi darasa la kumi na moja kwamba 1973.
    Mwalimu Mkuu wa SDkuli ya Sekondari ya Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja Mwalimu Haroun Juma akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara fupi kuangalia maendeleo ya changamoto zinazoikabili Skuli hiyo.
    Balozi Seif akibadilishana mawazo na walimu wa Skuli ya Kinyasini Sekondari alipokfanya ziara fupi skulini hapo.
    Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kinyasini Sekondari Haroun Juma akimuonyesha Balozi Seif Vikalio vilivyotengenezwa kwa zege ndani ya madarasa ya Sekondari ya skuli hiyo.
    Balozi Seif akishangaa mabadiliko makubwa ya majengo ndani ya Skuli ya Sekondari ya Kinyasini ambapo ndipo alipoanzia kupata elimu ya msingi katika miaka ya 46. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Skuli ya Kinyasini Sekondari Nd. Simba Haji.
    Balozi Seif akiangalia kisima cha Skuli hiyo ambacho kilipata hitilafu ya mafuta baada ya bomba la mafuta lka kituo cha Petroli kiliopo katibu na skuli hiyo kupasuka na kutembea katika miamba hadi eneo hilo la kisima. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo ya Kinyasini Sekondari Mwalimu Haroun Juma.
    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizunguma na wazazi, kamati ya skuli, walimu na wanafunzi wa skuli ya sekondario ya Kinyasini mara baada ya kukaguzwa kuona maendeleo na chngamoto zinazoikabili. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.