ufupi
Wengi huanza kuchakaza
viatu vyao wakipita ofisi moja baada ya nyingine kuomba nafasi za kazi
zilizotangazwa na mwishowe hujikuta wakiwa wamefanya usaili zaidi ya ofisi 10
pasipo kuitwa kazini.
Kwa
kawaida vijana wengi Afrika, hususan Tanzania wanapohitimu elimu ya juu, jambo
ambalo hulifikiria ni kutafuta ajira.
Wengi
huanza kuchakaza viatu vyao wakipita ofisi moja baada ya nyingine kuomba nafasi
za kazi zilizotangazwa na mwishowe hujikuta wakiwa wamefanya usaili zaidi ya
ofisi 10 pasipo kuitwa kazini.
Hata
hivyo hii ni tofauti na msanii wa
Hip
Hop kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon maarufu kama Nikki wa II ambaye ana
shahada ya Uzamili katika maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDMS).
Nikki
wa II ambaye pia ni mshindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro 2014 KTMA kupitia
wimbo Bora wa Hip Hop “Nje ya Box”, aliowashirikisha G Nako na Joh Makini wote
kutoka Kundi la Weusi, anasema licha ya kwamba amehitimu elimu ya juu na kupata
alama kubwa, hayupo tayari kuajiriwa.
Rapa
huyu ambaye ni mdogo wa damu wa mwanamuziki John Simon maarufu kama Joh Makini
wiki hii ameachia wimbo wake mpya “Sitaki Kazi” wimbo ambao umebeba maudhui
makubwa yenye kutoa elimu kwa vijana wa rika na elimu za aina
zote.
Msanii
huyu aliyeibukia katika fani mwaka 2008 na wimbo wake “Good Boy” aliokuwa
amemshirikisha Rama Dee, anasema hisia alizonazo ndizo zilizomfanya atunge
mistari ya wimbo huo, kutokana na maisha halisi ya vijana wa
sasa.
“Niliimba
wimbo huu kutokana na kuwaona vijana wengi wenye elimu ya juu wakihangaika
kupita huku na kule na vyeti vyao wakitafuta ajira, kwangu mimi naona ni utumwa
kwa msomi kutegemea kufanya kazi za watu wengine, badala ya kuibua cha kwako ili
utoe ajira kwa wengine,” anasema.
Hata
hivyo anabainisha kuwa namba ya vijana wanaohitimu stashahada, shahada ya kwanza
na kuendelea inazidi kuwa kubwa na ajira ni za
kubahatisha.
“Ndani
ya mistari ya wimbo “Sitaki Kazi” kuna mistari inayoelezea namna kijana
anavyoweza kutatua tatizo la ajira kwa kubuni vitu mbalimbali ambavyo
vitazalisha pato na kuweza kuajiri maelfu ya vijana wanaohitimu mwaka hadi
mwaka,” anasema rapa huyo.
Anasema
ingawa nchi haina utaratibu maalumu wa kuwaandaa vijana pindi watakapomaliza
elimu zao, kuna haja ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili kwa vijana
husika.
“Tatizo
kubwa katika nchi yetu hakuna mtu au utaratibu ambao unawaandaa vijana, lakini
sisi wenyewe lazima tutambue kwamba hii ni karne ya kutengeneza ajira yetu
wenyewe, ndiyo maana nimeimba wimbo huu ili kubadilisha mtizamo na fikra za
vijana ambao wanategemea ajira, ni lazima jamii ibadilike,” alisema Nikki wa
II.
Nikki
anasema katika usanii alionao anajivunia kufanya kazi hiyo kwani ni kujiajiri
inayomwingizia kipato kikubwa ukilinganisha na ajira ya ofisini ambayo ingembana
na asingeweza kupata fedha ya ziada nje ya
mshahara.
Anasema
hiyo inamfanya avutiwe na kazi yake kwani anaamini kwamba elimu inamsaidia
kuiboresha kazi yake, hivyo anaitumia kuongeza ujuzi katika muziki na kazi
mbalimbali za Kampuni ya Weusi.
“Kijana
lazima ujiamini kwamba unaweza kutengeneza ajira, watu ninaowapenda na maarufu
walifanya kazi katika jamii na kutoa ajira kwa vijana wangakuwaje iwapo Biliget
angeajiriwa, inakuwaje Bhakresa au Mohamed Dewji wangeajiriwa? Leo hii maelfu ya
Watanzania wasingekuwa na ajira,” anasema.
Anasema
kiuna mambo mengi aliyoyazungumzia katika wimbo huo ikiwamo ubunifu kwa
kuwahamasisha vijana wawe wabunifu ili kukuza nafasi za ajira na kuongeza pato
la taifa.
“Sitafuti
kazi ila nataka nitafutwe na watu wanaotafuta kazi’, haya ni moja ya mashairi
yaliyopo katika wimbo huu ambao niliimba nikiwa na nia ya kuwahamasisha vijana
wawe wabunifu ili elimu tulizozipata tuweze kuzitumia katika kukuza uchumi wa
nchi na kujiendeleza sisi na familia zetu,” anasema rapa
huyo.
Nikki
wa II anatoa wito kwa vijana kujituma wao wenyewe kabla ya kufukuzwa kazi, kwani
wengi wao waliweza kufanya makubwa baada ya kufuzwa katika kazi za
kuajiriwa.
Anasema
ni vyema vijana wakajituma wao wenyewe kwa kufanya vile wanavyovipenda kuliko
kufanya kazi wasizozipenda kwa kutumikia mishahara.
“Wengi
wanafanya kazi wasizozipenda kwa kutumikia mishahara, mtu anafanya kazi ili
apate mshahara na hii inasababisha wengi kulipua kazi na wakati mwingine
kutotekeleza majukumu yao ya kikazi.”
“Iwapo
mtu atafanya kazi anayoipenda au kujiajiri hujikuta akifanya kazi mpaka usiku wa
manane na hapo tayari anakuwa ametengeneza pato kubwa kwake au kampuni yake
kwani anafanya kitu chenye masilahi kwake na siyo kwa kampuni fulani au mtu
binafsi,” anasema Nikki wa II.
Licha
ya kutoa darasa hilo kwa wasomi nchini, rapa huyo alirudi pia kwa watu wa
uswahilini na wale wasio na elimu na kuwataka kutokata tamaa na kuishia kuomba
ajira kwa watu wengine kwani na wao wana nafasi kubwa ya kujituma na kumiliki
makampuni makubwa.
“Mimi
nimezaliwa uswahini huko Arusha, ninavyojua mimi watu wengi wa huko hawana CV
wala vyeti, ndani ya wimbo huo kuna mistari nimeimba kwa ajili yao,”
anasema.
Kuhusu
Nikki wa II
Kijana
huyu mzawa wa Daraja Mbili Arusha, alisoma Arusha Sekondari. Nikki anafahamika
zaidi kwa kazi zake kama Good Boy, Nje ya Box, Gere, Pea, Kiujamaa, Bum Kubam na
nyinginezo.
0 comments:
Post a Comment