May 22, 2014

  • Hatari nyingine mpya ya bakteria kwenye ndege za kusafiria

     
     
     
     
    Screen Shot 2014-05-21 at 4.08.31 PM
    Ripoti imetolewa ikionyesha sehemu gani ndani ya ndege inalea vijidudu vya bakteria zaidi ikiwemo ile sehemu ya kuwekea mkono katikati ya viti, kwenye vidirisha pamoja na sehemu ya nyuma ya kiti panapotumika kuweka vitu mbalimbali.Wachunguzi wa Chuo cha Auburn nchini Marekani wamefanya uchunguzi ili kujua ni sehemu gani ndani ya ndege inalea na inaruhusu vijidudu vinavyosababisha maambukizo ya magonjwa mbalimbali likiwemo gonjwa kali ya E.Coli.Uchunguzi waliufanya ndani ya ndege ya Delta Airlines ambayo hufanya safari zake nchini humo.

    Screen Shot 2014-05-21 at 4.09.44 PM
    Bakteria anaesababisha ugonjwa wa E.Coli ambao bado sijapata maelezo yake ya kitaalamu jinsi unavyoathiri mwili wa mwanadamu, anaweza kuishi mpaka siku 7 kwenye meza za kulia chakula ndani ya ndege ambapo kwa kipindi hiki unaambiwa ni hatari na kwa binadamu na ndio anatumia hiyo time kuusambaza.
     
    Wachunguzi hao wameshauri watu kunawa mikono mara kwa mara na kutumia dawa za kusafishia mikono ambazo zinatumika kuulia bacteria yaani anti-bacterial.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.