Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni – FIFA
Sepp Blatter amesema ilikuwa kosa kuichagua Qatar kuandaa dimba la Kombe la
Dunia mwaka wa 2022 kwa sababu ya hali ya joto kali nchini humo
Blatter amekiambia kituo kimoja cha
televisheni nchini Uswisi kuwa, na namnukuu “unajua, kila mmoja hufanya makosa
maishani”.
Kiwango cha wastani cha joto ni nyuzijoto 40
katika miezi ya Juni na Julai, kipindi ambacho tamasha la kombe la dunia
hupangwa kufanyika.
Blatter amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa
dimba hilo la mwaka wa 2022 litaandaliwa katika msimu wa baridi. Wakati huo,
kiwango cha joto hufikia nyuzijoto 25.
Hata hivyo rais huyo wa FIFA hakuzungumza
lolote kuhusu madai ya rushwa kuhusiana na mchakato wa kupiga kura uliosababisha
Qatar kuchaguliwa kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.
Hata hivyo amesema kulikuwa na shinikizo kubwa
la kisiasa kutoka Ufaransa na Ujerumani.
Wakati huo huo, Brazil inakabiliwa na mtihani
wa maandalizi yake ya usalama kwa ajili ya michuano ya dimba la Kombe la
Dunia.
Wananchi wanaokasirishwa na gharama kubwa za
kuandaa michuano hiyo wiki hii walifanya maandamano ya kupinga gharama
zinazotumiwa katika maandalizi ya tamasha hilo pamoja na migomo ya wafanyakazi
katika miji kadhaa mikubwa nchini humo.
Maelfu ya walimu waliandamana katika mji wa
Sao Paulo takriban kwa wiki nane sasa wakidai kulipwa mishahara mizuri na kuwepo
kwa mazingira mazuri ya kazi.
Migomo ya kazi inayoendelea kufanywa na walimu hao na polisi
na tishio la kufanyika kwa mgomo wa taifa zima na polisi pia inazusha hofu ya
vurugu ikiwa zimebakia wiki nne tu kabla ya kuanza kwa michuano ya soka Kombe la
Dunia.
Jumla ya watu 10,000 wamendamana katika mitaa
ya mji wa Belo Horizonte, Barasilia mji mkuu wa Brazil, Manaus, Porto Alegrea,
Rio na Sao Paulo.
Katika mji mkuu wa kibiashara wa Sao Paulo
takriban wanachama 5,000 wa Vugugu la Wafanyakazi wasiokuwa na Makaazi waliwasha
matairi ya magari na kuandamana hadi katika uwanja wa Corinthians Arena ambapo
ndipo patakapofanyika pambano la ufunguzi kati ya Brazil na Coatia hapo Juni 12.
Huyu hapa mmoja wa waandamanaji.
Chanzo: DW kiswahili
0 comments:
Post a Comment