Na Nathaniel Limu, Singida
MAKAMPUNI yanayojishughulisha na tafiti mbali
mbali za nafaka yameshauriwa kuongeza juhudi zaidi ili kupata mbegu bora
zitakazowasaidia wakulima kupata chakula cha kutosha na kujikomboa
kiuchumi.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Diwani wa
Kata ya Mwasauya (CCM) tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida, Seleman Ntandu
wakati akizungumza kwenye kilele cha sherehe za wakulima wa kata ya Ikhanoda na
Mwasauya.
Amesema ili kilimo kiweze kuwa na tija kwa
wakulima hasa wakati huu ambao dunia inapambana na majanga mengi
yanayosababishwa na tabia nchi, ni lazima watumie mbegu bora na zilizofanyiwa
utafiti wa kina.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Namburi
inayozalisha mbegu za mtama na uwele,Dk.Andrew Peter Mgonja akizungumza kwenye
kilele cha sherehe za wakulima wa vijiji vya Ngamu na Mwasoiya wilaya ya
Singida.Wa tatu kulia (waliokaa) ni Diwani wa kata ya Mwasoiya Selemani Ntandu
na wa pili ni Mwenyekiti wa kijiji cha Mwasoiya.Picha zote na Nathaniel
Limu.
“Kwa hiyo, ndugu Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Namburi inayozalisha mbegu za mtama na uwele nakuomba usichoke
kufanya utafiti zaidi ili kampuni yako iweze kupata mbegu bora zaidi
itakayowasaidia wakulima kuondokana na njaa na wakati huo huo wajiongezee kipato
kwa kuuza mazao ya ziada”,alifafanua.
Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya kuzalisha mbegu
za mtama na uwele ya Namburi ya mjini Arusha, Dk. Andrew Peter Mgonja amewataka
wakulima kutumia mbegu za mtama na uwele zinazozalishwa na kampuni yake kwa
madai kwamba zinakabiliana na ukame uliopo kwenye mikoa ya kanda ya
kati.
Diwani wa kata ta Ikhanonda
jimbo la Singida kaskazini,ikitoa nasaha zake katika kilele cha sherehe za
wakulima wa vijiji vya Ngamu na Mwasoiya.Pia aliwahamasisha kuboresha
utengenezaji wa pombe ya kienyeji ya mtukuru ili ianze kuhifadhiwa kwenye
chupa/pakiti ili iuzwe ndani na nje ya mkoa.
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, amesema mbegu
aina ya naco mtama one (1) ambayo tarafa ya Ilongero imeipa jina la Dk. Parseko
Kone kwanza kwa eka moja inatoa gunia 13 ikilinganisha na gunia 4 za mtama wa
kienyeji.
Mkurugenzi wa
kampuni ya uzalishaji wa mbengu bora ya Namburi,Dk.Andrew Peter Mgonja (kushoto)
akikagua shamba darasa la kijiji cha Mwasoiya wilaya ya Singida.Kulia ni afisa
kilimo wilaya ya Singida,Sankwera.
“Naco mtama (1), inakomaa kwa kipindi cha
miezi miwili tu wakati mtama wa asili unakomaa baada ya miezi sita. Ina soko
kubwa kwenye makampuni yanayotengeneza bia na mabua yake yana mafuta ambayo
yanayoweza kuendesha mitambo mbalimbali”, alifafanua Dk. Mgonja.
0 comments:
Post a Comment