July 21, 2014

  • REAL MADIRID YAIPIGA KIKUMBO MAN UNITED NA KUIWEKA SOKONI JEZI YA JAMES RODRIGUEZ


    REAL MADIRID YAIPIGA KIKUMBO MAN UNITED NA KUIWEKA SOKONI JEZI YA JAMES RODRIGUEZ

    Manchester United, Real Madrid, James Rodriguez,                    Monaco, Colombia, World Cup, Golden Boots, Cristiano                    Ronaldo, Gareth Bale, Liverpool

    REAL MADRID imeonyesha kujiamini na dili la kumsajili mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez baada ya kuiweka jezi ya nyota huyo kwenye duka lao la klabu.

    Jina James likiwa na namba 10 mgongoni limeonekana kwenye jezi ya Real Madrid itakayotumika msimu ujao.

    Iliripotiwa mapema kuwa Real Madrid ina uhakika wa kumnasa Rodriguez na kwamba tayari ilishaanza kumtafutia nyumba yeye na familia yake kwenye jiji la Madrid.

    Manchester United ilikuwa tayari kulipa pauni milioni 63 kwa mshindi huyo wa kiatu cha dhahabu cha Kombe la Dunia lakini vyombo vya habari vya Hisapania vimedai Real Madrid imeshaafikiana na mkali huyo pamoja na wakala wake na kwamba kilichobakia sasa ni kumalizana  na Monaco.

    Rodriguez mwenye amedaiwa hataki kucheza mchezo wowote wa kirafiki kwa timu yake ya Monaco kwa kuhofia kuumia na kupelekea kutibua dili lake la kwenda Real Madrid.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.