Na Anna
Nkinda – Maelezo
Wilaya ya
Kinondoni kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaandaa
mkakati wa kusafirisha wanafunzi kwa vitambulisho maalum vya wanafunzi kwa bei
naafuu kwa kutumia mabasi ya UDA kwenda shule za pembezoni.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kinondoni Omath Sanga
wakati akisoma taarifa ya Idara ya Elimu kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
alipoitembelea shule ya Sekondari ya Kata ya Salma Kikwete iliyopo Kijitonyama
wilayani humo.
Sanga alisema
wanafunzi hao ambao wanatumia usafiri wa mabasi zaidi ya moja kwenda shule kwa
siku kutoka majumbani kwao kuelekea maeneo ya Goba, Fahari, Kinzudi, Mabwe,
Kisauke, Njechele, Mabibo, Malambamawili, Hondogo, Gogoni, Kibwegere na
Kibweheri mara baada ya kukamilika kwa vitambulisho bivyo watalipa nauli ya
shilingi 200 kwenda na 200 kurudi.
“Mwanafunzi
atatumia kitambulisho maalum ambacho kitamuwezesha kupanda zaidi ya basi moja la
UDA kutoka nyumbani hadi kufika shuleni kwa gharama ya shilingi 400 kwa siku
hii ni kwenda na kurudi tofauti na ilivyo sasa wanatumia fedha nyingi katika
nauli kwani tatizo la usafiri kwa wanafunzi limekuwa ni moja ya changamoto
inayoikabili wilaya yetu”, alisema Sanga.
Aidha alisema
changamoto zinazoikabili idara hiyo ni upungufu wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia, walimu wa masomo ya sayansi kwa shule za sekondari, vyumba vya
madarasa, madawati na maabara kwa baadhi ya shule za msingi na Sekondari na
ukosefu wa usafiri kwa wanafunzi wanaosoma shule za
pembezoni.
Alisema
mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo ni wilaya hiyo imekuwa ikitenga
bajeti kila mwaka kwa ajili ya ununuzi wa madawati, ujenzi wa vyumba vya
madarasa pamoja na kukabiliana na uharibifu wa miungombinu. Vilevile
wanashirikiana na wanajamii kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa
madawati.
Kwa upande
wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) aliwataka wanafunzi hao kuitumia Sayansi na Teknolojia kutafuta elimu na
siyo tofauti kwani Dunia ya leo inahitaji mtu mmoja kuwa na utaalam wa namna
nyingi ili aweze kufanikiwa na kuwa kivutio katika soko la ajira na
kujiajiri.
Vilevile
kuweza kwenda na wakati kulingana na mabadiliko jambo la muhimu ni kutokata
tamaa mapema na kutojiweka nyuma kwenye elimu yoyote yenye faida
maishani.
Mama Kikwete
alisema lengo kuu la elimu ni kuhakikisha mwanadamu anapata maendeleo endelevu
katika maisha yake ya uzima wa sasa na wa abaadaye, ili kuweza kulinda na
kudumisha utu wake pamoja na kuendelea kuimarisha hazi zake za msingi kwani
maisha ya mtu aliyesoma ni tofauti na maisha ya mtu
asiyesoma.
“Kila mtu
anapaswa kuhakikisha kuwa elimu anayoipata inamsaidia kuchangia maendeleo ya
jamii husika, sanjari na kukua uelewano, uvumilivu na urafiki kati ya watu wa
mataifa mbalimbali na kwa njia yah ii wau wanaweza kujenga misingi ya haki na
amani”, alisema Mama Kikwete.
Akiongea kwa
njia ya simu Mwenyekiti Mtendaji wa UDA Robert Kisena alisema vitambulisho hivyo
ni maalum kwa ajili ya wanafunzi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es salaam
ambazo ni Ilala, Temeke na Kinondoni wanasoma shule za Sekondari zilizopo
pembezoni mwa mji.
“Wanafunzi
watakaotumia vitambulisho hivi ni wale wanaotoka umbali wa km 30 hadi km 60
kutoka nyumbani hadi shuleni ingawa katika makubaliano ya awali ilikuwa ni
walipe nauli ya shilingi 200 na kwa wanafunzi wasio na uwezo wasilipe nauli
lakini kampuni yangu itaangalia kama ikiwezekana wasilipe nauli
kabisa.
Tatizo la
usafiri kwa wanafunzi wanaotoka Buguruni hadi Ubungo ni tofauti na kwa
mwanafunzi anayetoka Buguruni hadi Chanika hawa wa chanika wanatumia mabasi
zaidi ya moja na kulipa nauli kubwa, lakini mwanafunzi akiwa na kitambulisho
hiki ataweza kupanda mabasi ya UDA hata matatu kwa gharama ya shilingi 200 tu”,
alisema Kisena.
Kisena
alisema wanafunzi hawa watatumia vitambulisho hivyo wakiwa wamevaa nguo za shule
hata kama ni mwishoni mwa wiki na tayari picha za wanafunzi 13,000 kutoka wilaya
zote tatu zimeshapokelewa katika ofisi za UDA kwa ajili ya utengenezaji wa
vitambulisho.
Alisema
gharama za utengenezaji wa vitambulisho ni za aina 2 kuna vya shilingi 1000 na
4500 wanachosubiri ni jibu kutoka Serikali ya mkoa ili iweze kuchagua aina gani
ya vitambulisho vitengenezwe kwani gharama ya utengenezaji wa vitambulisho siyo
za UDA.
Wilaya ya
Kinondoni ina jumla ya shule za Msingi 236 kati ya hizo 140 ni za Serikali
ambazo zinawanafunzi 152,426 na shule binafsi 96 zenye wanafunzi 29,101. Shule
za Sekondari ni 137 kati ya hizo 46 ni za Serikali na 91 ni za binafsi. Idadi ya
wanafunzi katika shule zote za Serikali ni 44,621 kati ya hao wavulana ni 23,466
na wasichana ni 21,155.
0 comments:
Post a Comment