SHULE ya Sekondari ya Pugu, iliyopo maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam, ambayo inasifa kubwa nchini kwa kuwa iliwahi kufundishwa na Baba wa Taifa, hayati Julius Kambarage Nyerere, imevamiwa na wadudu aina ya kunguni ambao wanadaiwa kuwasumbua wanafunzi wa bweni wa shule hiyo.
Akizungumza na paparazi, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Agustino Angelo, alisema tatizo hilo limekuwepo muda mrefu na wamejitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa kwa kufanya upuliziaji (fummigation) mara mbili huku naye Mstahiki Meya wa Ilala Jerry Slaa, akiahidi kulimaliza kabisa tatizo hilo katika siku za hivi karibuni.
Paparazi alizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, ambao walikiri kusumbuliwa na tatizo hilo ambalo wanadai kuwa linawakosesha amani na kuwataka viongozi wa serikali wajitokeze kutokomeza tatizo hilo ili waendelee na masomo yao vizuri.
Mbali na hayo, paparazi pia alishuhudia majengo chakavu ya shule hiyo, mazingira ambayo si rafiki na heshima ya shule hiyo yenye historia kubwa nchini ambapo inasemekana kuwa tatizo hilo ni la mda mrefu sana kwana hata wanafunzi wa kipindi cha nyuma tatizo la kunguni lilikuwepo tangu miaka ya 2000.
0 comments:
Post a Comment