May 25, 2014

  • MASHABIKI WA MADRID ZAIDI YA 80,000 WAMEJITOKEZA KUANGALIA FAINALI YA UEFA UWANJANI KWAO




    MASHABIKI WA MADRID ZAIDI YA 80,000 WAMEJITOKEZA KUANGALIA FAINALI YA UEFA UWANJANI KWAO

    Zaidi ya mashabiki 80,000 wamejitokeza kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid wamejitokeza kuangalia mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Ingawa fainali hiyo ilikuwa inachezwa jijini Lisbon, Ureno, mashabiki hao walijitokeza kwa wingi kwenye uwanja wao wa nyumbani.
    Hata hivyo walilazimika kukaa kimya kwa dakika 90 kutokana na Atletico Madrid kuwa kiwembe na kupata bao mapema.
    Segio Ramos alisawazisha kabla ya Bale, Marcelo na Ronaldo kufunga mengine matatu na kuzaa matokeo ya ushindi wa mabao 4-1.
    Real Madrid wamechukua kombe la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.