May 12, 2014

  • Howard University yamtunuku P.Diddy shahada ya uzamivu ya heshima 'doctorate', sasa ni Dr. Sean Combs

     

    Mwanahip pop tajiri zaidi duniani, Sean Combs aka Puff Daddy/P.Diddy amepiga hatua kubwa ya heshima baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya uzamivu 'doctorate' na chuo kikuu cha Howard, Jumamosi (May 10).
    Rapper huyo alionekana mwenye furaha sana tangu akiwa njiani kuelekea kwenye sherehe hizo ambapo alianza kutupia picha kwenye Instagram na kuiambia dunia jinsi anavyojisiki.
    "I'm not known for sleeping, and it's very hard for me to wake up..I'm not a morning person! Today my wake up call was 6:30am I been up since 5am!!! Dancing to James Brown and getting ready for this special day! I ain't need no wake up call today jack!! #DiddySpeechHU."
    Dr. Sean Combs alipost jumbe mbalimbali akieleza jinsi chuo kikuu hicho kilivyoyabadilisha maisha yake kwa ujumla na kuwatia moyo watu wengine pia.
    "Howard University didn't just change my life--it entered my soul, my heart, my being and my spirit…Nobody is going to invite you to the front of the line, you got to push your way to the front of the line."
    Kwa mujibu wa Billboard, rapper huyo aliwahi kusoma Howard University hapo awali akichukua masomo ya biashara lakini aliacha chuo mwaka 1990 baada ya kusoma miaka miwili tu.
    Dr. Sean Combs alitunukiwa shahada hiyo Jumamosi pamoja na mtangazaji wa CNN Wolf Blitzer, daktari wa upasuaji Clive Callender, na mpiga saxophone Benny Golson na Co CEO wa Pepsi, Indra Nooyi.

    "Tunayo heshima kuwa na Mr. Combs kama msemaji wetu. Alikaa kwenye madarasa ambayo wanafunzi wetu wanakaa, alitembea umbali, na kama wanafunzi wengi, spirit yake ya ujasiriamali ilisambaa Howard." Alisema Wayne Frederick ambaye ni rais wa Howard kwa muda huu.

    "Ain't no homecoming like a Howard homecoming…and it feels so goog to be home." Alisema Diddy wakati akitoa hotuba baada ya kupewa degree ya humanity. 

    Inawezekana rapper huyo akabadili tena jina la career yake ambalo mwezi March alilifanyia marekebisho na kurudi kwenye Puff Daddy,  huenda sasa atataka afahamike kama Dr. Combs.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.