July 25, 2014

  • MERIAM IBRAHIM SASA HURU DHIDI YA WATESI, AELEKEA ROMA KUMSABAHI PAPA




    MERIAM IBRAHIM SASA HURU DHIDI YA WATESI, AELEKEA ROMA KUMSABAHI PAPA

    Waziri wa mambo ya nje ya Italia, Lapo Pistelli kwenye 'selfie' (picha aliyojipiga) na Meriam, ambapo kwenye mtandao aliandika, 'Mission Accomplished', yaani 'kazi imekamilika.' ©Premier Christian Radio
    Hatimaye jasho la haki limepatikana, ambapo Meriam Yahia Ibrahim Ishag, mwanamke aliyepata suluba kutokana na imani yake ameachiwa huru baada ya Vatican kuelezwa kufanya mazungumzo ya chini kwa chini na Sudan na hatimaye kufikia makubaliano.

    Meriam amenusuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Italia, Bwana Lapo Pistelli, ambapo hadi kufikia saa kumi alfajiri siku ya Alhamisi, ndege binafsi ilipaa kuelekea Italia, familia ya Meriam ikiwa ndani.

    Mara baada ya kufika Roma, Papa Francis ambaye alifurahia uwepo wa watoto wa Meriam na kucheza nao, alimpongeza Meriam kwa kutetea imani na kutotetereka. Kituo cha TV cha Italia kilionyesha ndege iliyombeba ikitua, na kueleza kwamba Meriam alionana Papa kwa ajili ya mazungumzo kwa nusu saa katika makao makuu ya papa Santa Marta Vatican, kabla ya kuelekea nchini Marekani.

    Meriam alihukumiwa kifo baada ya kudaiwa kuikana dini ya Kiislamu na kuwa Mkristo, japo katia maelezo yake ameeleza mara kadhaa kwamba hajawahi kuwa Muislamu, kwani baba yake (ambaye ndiye alikuwa Muislamu) aliitelekeza familia ya kumuachia mama ambaye alikuwa mkristo.



    Akiwa kifungoni, Meriama lilazimika kujifungua mtoto wake wa sasa huku akiwa amefungwa kwenye minyororo, jambo ambalo limeelezwa kumsababishia mtoto huyo ulemavu.


    Juni 23, Mahakama ya rufaa ilitengua hukumu ya Meriam, na hivyo kumuweka huru, japo maofisa usalama walimkamata upya akiwa uwanja wa ndege kuelekea nchini Marekani, ambapo walieleza kwamba wanakagua hati za kusafiria ambazo zimefojiwa.

    Baada ya tukio hilo Meriam aliachiwa na akapata hifadhi kwenye ubalozi wa Marekani, ambapo ndugu zake walimfungulia kesi upya hadi aliposafiri kwenda 'kumsabahi Papa' kabla ya safari ya Marekani, ambako mume wake ana uraia wa nchi hiyo.

    Meriam akiwa na watoto wake nchini Italia.





  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.