Waziri Mkuu wa zamani wa
Malaysia amesema Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani CIA linaficha maelezo
muhimu kuhusu hatima ya ndege ya Malaysia iliyotoweka. Katika taarifa
aliyochapisha katika weblogu yake siku ya Jumapili, Mahathir Mohammad amesema
CIA na shirika la utengenezaji ndege la Marekani, Boeing, kwa pamoja zinaficha
maelezo kuhusu ndege iliyotoweka. Aidha amesema ni jambo la kushangaza kuona
vyombo vikubwa vya habari duniani havifuatlii kwa kina kadhia ya ndege hiyo ya
Malaysia. Mahathir amesema yamkini CIA iliongoza ndege hiyo kwa mbali na kuiweka
katika mfumo wa kujiendesha yenyewe kisha ikatua eneo la siri na alama zake za
Malaysian Airlines kuondolewa. Ndege hiyo ya Shirika la Ndege
la Malaysia iliyotoweka tarehe 8 mwezi wa Machi mwaka huu ikiwa na mamia ya
abiria ilipokuwa inaelekea Beijing, China kutoka Kuala Lumpur Malaysia. Pamoja
na kuwa nchi kadhaa zinashirikiana katika juhudi za kuitafuta ndege hiyo kwa
kutumia teknolojia ya kisasa lakini bado hakuna athari zozote za ndege hiyo ya
kisasa aina ya Boeing 777-200ER iliyotengenezwa Marekani. Waziri Mkuu wa
Malaysia Najib Razak naye pia alinukuliwa akisema ndege ya abiria ya nchi hiyo
iliyotoweka ilipotoshwa mkondo wake kwa makusudi na kuendelea kuruka angani
masaa kadhaa hata baada ya kutoweka kwenye
rada.
0 comments:
Post a Comment