BAADA ya ukungu kutanda Yanga SC kufuatia kutimka kwa wachezaji Kavumbagu na Frank Domayo, hatimaye Mwenyekiti wa klabu Yussuf Manji (pichani) amenena jambo.
Manji amesema kuondoka kwa wachezaji hao sio mwisho wa timu ya Yanga, kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya kuhakikisha inasajili wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye msimu ujao kwa kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Yanga (www.youngafricans.co.tz), Manji katika mazunguzo yake na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, alisema: "Yameongelewa mengi sana kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao sikuwepo nchini kwa ajili ya kazi zangu binafsi lakini sasa nimerejea na maandalizi ya msimu ujao yameshaanza."
Amedai kuondoka kwa Kavumbagu ni kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji wageni kwa msimu mpya, huku Domayo ambae tangu mwaka jana aliombwa kuongeza mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya hivyo.
Pamoja na kuondoka kwa wachezaji hao bado kwa kushirikiana na kocha aliyeoondoka (Hans) watahakikisha Yanga inaendelea kutisha msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.
Wakati akiongea na waandishi wa habari kwaajili ya kuiaga Yanga, Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia klabu.
Aidha, Manji amelifuta rasmi tawi la Tandale kutokana na kuwa na chanzo cha vurugu na migogoro ndani ya klabu, pia amewafuta uanachama wanachama sita ambao walikiuka katiba ya Yanga kwa kwenda kuongea na waandishi na habari bila ya Idhini ya uongozi huku pia wakishindwa kulipia ada zao za uanachama kwa zaidi ya miezi sita.
Wanachama hao waliofutwa uanachama ni Ally Kamtande, Isiaka Dude, Hamisi Matandula, Waziri Jitu Ramadhani, Mohamed Kigali Ndimba na Selaman Hassan Migali.
Mwenyekiti huyo akasema Mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba utafanyika terehe mosi Juni, 2014 katika Ukumbi wa Oysterbay Police Mess na wanachama wote wanaombwa kulipia ada zao ili waweze kuhuhudhira mkutano huo wakiwa hai.
Manji pia akasema suala la ujenzi wa Uwanja wa Kisasa eneo la Jangwani bado lipo pale pale, kikubwa kinachosubirwa ni majibu ya serikali juu ya maombi ya eneo la ziada, kwani Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alisema suala hilo lipo ukingoni na mada si mrefu.
0 comments:
Post a Comment