CHELSEA kumaliza msimu bila taji lolote ni jambo lisilokubalika kwenye akili ya mmiliki Roman Abramovich.
Soka lililokosa mvuto ni 'adui' miwngine wa Abramovich. malumbano ya kocha na wachezaji, kocha kukaripiana na waamuzi ni kero nyingine kwa tajiri huyo wa kirusi.
Yote haya yanatokea Chelsea chini kocha Jose Mourinho.
Inasemekana Abramovich yupo tayari kufutialia mbali mapenzi yake kwa Mourinho na hata kumtimua.
Abramovich alitarajiwa kuwepo uwanjani katika mechi iliyopita dhidi ya Norwich lakini akaingia mitini.
Amekuwa na kawaida ya kufanya hivyo pale anapotaka kuchukua maamuzi magumu. Hata wakati anataka kumtimua Carlo Ancelotti alisusa kwenda uwanjani.
Tajiri huyo anaona kama vile Mourinho haitendei haki himaya ya soka la kuvutia anayojaribu kuiejenga Stamford Bridge.
Mshauri mmoja wa Abramovich anasema wachezaji kama Mata, Oscar, Hazard, Willian, Schurrle, Luiz na Azpilicueta ni aina ya wachezaji wanataka kutandaza soka lakini Mourinho amekuwa hawatumi katika mfumo mzuri na mbaya zaidi alimsotesha benchi Mata na hatimaye kumpiga bei.
Hamtumii vizuri Luiz na pengine hatma ya mchezaji huyo iko mashakani.
Wiki chache zilizopita, Chelsea ilipokuwa kwenye hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, huku pia ikiwa kwenye nafasi ya kunyakua taji la Ligi Kuu, Abramovich alionekana kutojali mbinu za Mourinho, lakini baada ya kipigo cha Atletico Madrid na Sunderland kwenye uwanja wa nyumbani, kila kitu kikabadilika.
Abramovich hana hamu tena na mbinu za Mourinho na lolote linaweza kutokea katika 'ndoa' hii ya pili ya wawili hao.
Mmiliki huyo ambaye mpaka sasa kishabadili makocha mara tisa tangu ainunue Chelsea mwaka 2004, huwa hapepesi macho katika kutoa maamuzi magumu.
Abramovich amekerwa na faini aliyopigwa Mourinho kwa kosa la kitoto la kumkoromea refa katika mechi ya Sunderland iliyomaliza rekodi yake ya mechi 77 bila kufungwa Stamford Bridge.
Je Mourinho ataonyeshwa njia ya kutokea? Ni jambo la kusubiri.
Hawa ndio makocha waliopita Chelsea chini ya uumiliki wa Abramovich.
• Claudio Ranieri: 2004
• Jose Mourinho: 2004 - 2007
• Avram Grant: 2007 - 08
• Luiz Felipe Scolari: 2008 - 09
• Guus Hiddink: 2009
• Carlo Ancelotti: 2009 - 2011
• Andre Villas-Boas: 2011 - 12
• Roberto di Matteo: 2012
• Rafa Benitez: 2012 - 13
• Jose Mourinho: 2013 hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment