GWIJI wa Manchester United Paul Scholes anaamini kuwa klabu yake ilipaswa kumtupia jicho zaidi kiungo wa Bayern Munich Toni Kroos kwenye usajili wao kuliko Ander Herrera.
Scholes anaona kuwa Herrera aliyesajiliwa kwa pauni milioni 28 hajafikia uwezo wa Kross anayeitumikia Ujerumani kwenye kombe la dunia.
Scholes anasema kwa kumkosa Kroos, Manchester United itakuwa imepoteza nafasi ya kuwa na mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu.
"Napenda kumtazama Kroos," anasema Scholes, "Nadhani ni mchezaji wa aina yake.
"Napenda namna anavyomiliki mpira na anavyoudhibiti mchezo. Anaweza kutoa pasi na ana muono wa hali ya juu.
"Kross anaweza pia kufunga kutoka nje ya box. Natamani Man United ingemsajili.
Inafurahisha kuona United inasajili wachezaji wapya, lakini haijasajili mchezaji yeyote wa kiwango cha Kross."
0 comments:
Post a Comment