Kundi la
Muziki wa kizazi kipya lijulikanalo kama “Wadananda” limebahatika kuingia
mkataba na Record label mpya nchini Tanzania ya “Brainstormusic”. kampuni hiyo
inayomsimamia msanii maarufu wa kizazi kipya ” CPwaa” imeamua kujitanua na
kuanza rasmi kusimamia kazi na wasanii wa muziki,filamu,Michezo,
Michoro,Vinyago,Upigaji picha pamoja na fashion.
Wadananda
linalotengenezwa na vijana wawili “Kea Ahmedi kidato”(Customer Care) na “Natali
Ali Katolila” (Pengo) wameingia mkataba huo na Brainstormusic mwezi wa pili
mwaka huu na tayari hivi sasa wameshapikwa vizuri na wanategemea kuachia single
ya mpya chini ya usamimizi wa Label hiyo mwezi ujao.
Wadananda
waimeingia mkataba wa kurekodi album ya muziki, TV Shows, Filamu na Management
kupitia “Brainstormusic”. Hivi mpaka dakika hii tayari wameshakamilisha
Photoshoots,Nyimbo yao mpya, na taratibu za kushoot video ndio
zinaendelea.
Wadananda
watakua wasanii wa pili baada ya CPwaa kuingia mkataba na label hiyo ambayo
imedhamiria kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya burudani. Wasanii wengine ambao
wapo kwenye hatua za mwisho za kupitishwa na label hiyo ni chipukizi wawili ”
Nurdin” na “Feisal”. Tayari kampuni hiyo imeshaini kikundi kimoja cha ngoma za
asili na kwa sasa hivi bado wanapitia maombi mengi ya wasanii wa Hip Hop na
Bongo flava.
“…Tumepata maombi mengi sana na bado
tunapokea maombi kutoka wasanii mbalimbali Tanzania.Wengi ni wasanii wa Hip Hop
na tuko makini kuhakikisha tunafanya kazi na watu
wanaojitambua,wamedhamiria,wanajituma na wana vipaji. CPwaa alishatoka na sasa
hivi kinachofanyika nikumuweka vizuri kwenye ramani ya soko la kimataifa.
Wadananda wameshapikwa wameiva na sasa ni zamu yao kutoka. Watu wategemee vitu
vizuri kutoka kwao na Brainstormusic kwa ujumla. Kwa kuanzia tuu tunataka mwaka
huu at least tuwe tumeshaini wasanii au makundi matano.”…….ameongezea Talent
Manager wa Brainstormusic “Almah Aboubakar Salum”
0 comments:
Post a Comment