May 21, 2014

  • Kinana afanya makubwa Manyoni, azindua nyumba ya kisasa ya mfugaji aliyezinduka kwa sera za CCM



    1. Kinana akihutibia mkutano wa hadhara Manyoni Mjini
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, Mei 20, 2014, kwenye Viwanja vya Stendi mjini Manyoni, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nane mkoani Singida, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua mkoani humo.
    2. Nape akihutubia Manyoni Mjini
    Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo.
    2b. Wananchi mkutano wa hadhara Manyoni Mjini
    Wananchi wakishangilia kwenye mkutano huo.
    3.
    Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Heka Azimio, zaidi ya kilometa 20 kutoka mjini Manyoni jana Mei 20, 2014.
    4
    Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimkaribisha jukwaani Mbunge wa Manyoni Mashariki  kapten Mstaafu John Chiligati kuwaeleza ananchi alivyosimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo lake hususan kijiji hicho cha Heka katika kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo ya umeme na maji.
    5.
    Wanachama 28 waliopewa kadi zao za CCM na Kinana kwenye mkutano huo wa Kijiji cha Heka Azimio, wakila kiapo.
    6.
    Kinana na Nape wakiwa na viongozi wengine wa Manyoni kuungana na wanachama hao wapya  kula kiapo.
    IMG_2614
     Kinana akipewa zawadi ya zana za asili na mzee mmoja wa Kijiji cha Heka, wilayani Mnyoni.
    7. Kinana akimpa fundi tofali, ujenzi wa maabara shule ya Heka
    Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimpa tofali fundi aliposhiriki ujenzi wa maabara ya shule ya sekondaro Heka, Manyoni, Mei 20, 2014 wakati wa ziara hiyo.
    7b.
    Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai (kushoto) akimpatoa tofali Nape ili kumpatia fundi wakati wa kushiriki kwenye ujenzi wa chumba cha maabara ya shule hiyo ya Heka.
    8. Nape akimpa fundi tofali, ujenzi wa maabara shule ya Heka
    Nape akimpatia fundi tofali kwenye kushiriki ujenzi wa chumba hicho cha maabara katika shule hiyo ya Heka,  Mei 20, 2014.
    10. Kinana akizindua nyumba ya kisasa ya mfugaji Mihangwa wa Kijiji cha Heka Azimio
    Kinana akizindua nyumba ya mpya ya kisasa ya mfugaji Jonase Mihangwa wa Kijiji cha Heka, wilayani Manyoni ambye  ambaye amekuwa miongoni mwa wafugaji wa kuigwa kwa kuamua kuuza sehemu ya mifugo yake kubadilisha maisha yake ikiwemokujenga nyumba hiyo ya kisasa yenye umeme wa mionzi ya  jua.
    11. Kinana na ujumbe ake wakiwa kwenye nyumba ya kisasa ya mfugaji huyo wa Kijiji cha Heka Azimio
    Kinana na msafara wake wakiwa kwenye nyumba hiyo ya kisasa ya mfugaji huyo.
    13. Kinana akiwa na mfugaji Mihangwa Jinasa wa Kijiji Heka kuzindua nyumba ya kisaa ya mfugaji huyo
    Mihangwa (kulia) akienda kumuonyesha Kinana nyumba yake duni ya zamani alimokuwa akiishi kabla ya uamuzi wake wa kuuza sehemu ya mifugo yake na kujenga nyumba ya kisasa.
    14. Nyumba ya zamani ya mfugaji huyo wa Heka Azimio Manyoni
    Nyumba duni ya zamani ya mfugaji Mihangwa.
    14b. Mfugaji Mihangwa Jinasa (wapili kushoto) akimuonyesha Kinana baadhi ya ng'ombe waliosalia baada ya kuuza wengine  ili kujenga nyumba ya kisasa Kijiji cha Heka Azimio
    Kinana akiangalia mifungo ya Mfugaji Mihangwa iliyobakia baada ya kuuza mingine kwa ajili ya kujenga nyumba ya kisasa. Mihangwa  anasema aliamua kuuza Ng’ombe 200 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa.
    15. Kinana akishiriki ujenzi wa Uwanja
    Kinana akishiriki ujenzi wa Uwanja wa Jumbe ambao umefanyiwa ukarabati na Mbunge wa Manyoni, Kapteni Chiligati.
    16. Kinana akiwa katika mazoezi na Vijana wa Umiseta, kwenye Uwanja wa Jumbe, Manyoni 2
    Kinana (wapili kushoto) akishiriki mazoezi na vijana wanaoshiriki michuano ya UMISETA kwenye Uwanja huo wa Jumbe, alipowatembelea kuwaona na kushoriki ujenzi wa Uwanja huo.
    17. Kinana akiwa katika mazoezi na Vijana wa Umiseta, kwenye Uwanja wa Jumbe, Manyoni
    Kinana (wapili kushoto) akishiriki mazoezi na vijana wanaoshiriki michuano ya UMISETA kwenye Uwanja huo wa Jumbe, alipowatembelea kuwaona na kushoriki ujenzi wa Uwanja huo.
    18. Kinana akiwa katika mazoezi na Vijana wa Umiseta, kwenye Uwanja wa Jumbe, Manyoni 3
    Kinana (wapili kushoto) akishiriki mazoezi na vijana wanaoshiriki michuano ya UMISETA kwenye Uwanja huo wa Jumbe, alipowatembelea kuwaona na kushoriki ujenzi wa Uwanja huo.
    19. Mwanachama wa CCM ktk Shina mamba tisa tawi la CCM Mwembeni Manyoni, Mchungaji  Daniel Makavu akisoma risala kwa Kinana
    Mwanachama wa CCM ktk Shina mamba tisa tawi la CCM Mwembeni Manyoni, Mchungaji  Daniel Makavu akisoma risala kwa Kinana (watatu kushoto), aliyefika kwa balozi wa shina namba tisa akiwa katika ziara hiyo mjini Manyoni.
    20. Kinana akizungumza nyumbani ka mjumbe wa shina namba tisa
    Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza kwenye kikao maalum nyumbani kwa Mjumbe wa shina namba tisa, tawi la CCM Mwembeni, Daudi  Mwembwa, alipofika kwa balozi huyo.
    IMG_2623

     Kinana akimpongeza Balozi  wa Shina la CCM la Mwembeni, Manyoni Mjini, Daud Mwimbwa alipokwenda kumtembelea na kuambiwa wanachama wote wa shina hilo wamelipia ada zote hivyo kuwa wanachama hai. Kinana alimpongeza na kumwalika kwenye kikao cha juu cha chama hicho kitakachofanyika Mbeya hivi karibuni, kwenda kueleza  mbinu alizozitumia kuwashawishi wanachama wake kulipia ada kitendo ambacho katika ziara zake zote alizozifanya nchini hakijawahi kutokea kwa balozi zingine. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.