Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego
Gutierrez (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
tamthilia ya redio iitwayo ‘Kinga ya Moyo Wangu’ itakayoelimisha watanzania
kuhusu umuhimu wa bima jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mkazi wa
Kampuni ya BIMA inayotoa huduma za bima kupitia simu za mkononi, Christian
Karlander. Tamthilia hiyo itasikika katika vipindi vya Jahazi na Leo Tena vya
Clouds FM.
Meneja Mkazi wa Kampuni inayotoa huduma
za bima kupitia simu za mkononi ya bima Tanzania, Christian Karlander (kulia)
akionyesha kipeperushi wakati wa uzinduzi wa tamthilia ya redio iitwayo ‘Kinga
ya Moyo Wangu’ itakayoelimisha watanzania kuhusu umuhimu wa bima jijini Dar es
Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego
Gutierrez.
Meneja Usambazaji wa Kampuni inayotoa
huduma za bima kupitia simu za mkononi ya bima Tanzania, Donald Galinoma
(kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthilia ya redio iitwayo ‘Kinga ya
Moyo Wangu’ itakayoelimisha watanzania kuhusu umuhimu wa bima jijini Dar es
Salaam jana. katikati ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego
Gutierrez.
Na Damas
Makangale, MOblog Tanzania
KAMPUNI ya
simu za mkononi ya Tigo Tanzania, leo imezindua tamthilia ya ‘Kinga ya Moyo
Wangu’ itayokuwa inarushwa hewani kila siku kwa wiki nane na kituo cha
utangazaji cha Clouds FM ambacho kitatoa elimu na kuhamasisha watumiaji wa simu
za mkononi wa mtandao wa tigo kujiunga na bidhaa ya pona na Tigo
bima.
Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez amesema tamthilia
hiyo maridhawa yenye matukio ya kusisimua itawavutia wasikilizaji pamoja na
kuwaelimisha watanzania kuhusu manufaa ya bima.
“Kampuni
ya simu za mkononi kama Tigo ina wajibu katika kuwapatia wateja wake huduma na
bidhaa zenye gharama nafuu. Sambamba na jinsi teknolojia ilivyoweza kuleta
mageuzi katika namna ambavyo tunaweza kutuma na kupokea fedha barani
Afrika,”
“hivi sasa
tupo tayari kufanya hivyo kupitia bima ya simu. Tigo inayofuragha kuwa mstari wa
mbele katika hatua hii kubwa kwa ajili ya Tanzania, ukuaji wa uchumi wake na
maendeleo ya taifa nzima,” amesema Gutierrez.
Amesema
kwamba programu hiyo ya redio imefadhiliwa na benki ya maendeleo ya Umoja wa
Ulaya kwa ajili ya kuelimisha umma umuhimu na faida ya kuwa na bima wakati
wote.
Kwa upande
wake , Meneja Mkazi wa Bima Tanzania, Christian Karlander amesema kuwa tamthilia
hiyo itarushwa mara mbili kwa siku kwa muda wa wiki nane kupitia vipindi vya
Jahazi na Leo Tena.
“Mradi huu
umezinduliwa na Bima, Kampuni inayoongoza kwa kutoa bima kupitia teknolojia ya
simu za mkononi nchini Tanzania, ambayo inatoa huduma ya bima ya maisha nay a
kulazwa hospitalini jijini Dar es Salaam kupitia mtandao wa simu wa Tigo,”
amesema
Karlander
aliongeza kuwa takribani milioni 4.6 ambayo ni asilimia 19 ya watu wazima nchini
wamewekewa bima, lakini ni kupitia bima za waajiri wao au chini ya mikopo hata
hivyo, kiwango cha watanzania waliojiandikisha bima kwa hiari ni ndogo
sana.
“Jijini
Dar es Salaam, Bima imesajili zaidi ya wateja 500,000 baada ya miaka miwili tu
ya kuanza kufanya kazi nchini, na asilimia 79 ya wateja hao ni watu wenye vipato
chini ya dola 2.50 (shilingi 4,215) kwa siku,” aliongeza
Karlander
Alisisitiza kuwa bidhaa hiyo ya bima kuanzia
gharama ya shilingi 750 na kiwango cha juu ni shilingi za kitanzania 4,000 kwa
mwezi na Bima inalipa mpaka shilingi 600,000 pindi mteja anapolazwa hospitalini
au kufariki dunia.
0 comments:
Post a Comment