May 13, 2014

  • AUDIO: SIKILIZA WIMBO USIDHARU SIFURI ...KAZI NYINGINE MPYA YA MASHUJAA BAND



    AUDIO: SIKILIZA WIMBO USIDHARU SIFURI ...KAZI NYINGINE MPYA YA MASHUJAA BAND

    USIDHARAU Sifuri ni kazi nyingine tamu kutoka kwa Mashujaa Band, washindi wa tuzo tatu za Kili Music.

    Ni wimbo mpya utunzi wake Rais wa bendi, Chaz Baba ambapo ndani yake anakwambia sifuri ikakaa mbele inafilisi, ikikaa nyuma inaongeza.
    Ni wimbo uliobeba ujumbe nzuri ndani yake, maudhui yake yakiwa yamelenga kwenye namna watu wanavyodhulumiwa mali za uridhi.
    Karibu kila mwimbaji ametupia pande zuri, huku marapa nao wakiachia mashambulizi ya nguvu.
    Wimbo umerekodiwa Sofia Production chini ya Ababuu mwana Zanzibar.
    Usidharau Sifuri ni moja kati ya nyimbo mbili mpya za Mashujaa zilizoachiwa wiki hii. Mwingine ni “Kiu ya Haki” ambao tuliutanguliza jana hapa Saluti5.
    Usikilize wimbo “Usidharau Sifuri” hapo chini.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.