May 13, 2014

  • CHELSEA KUMTOA LUKAKU KAMA CHAMBO CHA KUMNASA DIEGO COSTA




    Bait: Lukaku, on loan at Everton this term, could be used in a deal to bring Diego Costa to Chelsea
    MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Romelu Lukaku aliyeichezea Everton kwa mkopo msimu huu ulioisha, atapelekwa Atletico Madrid kama sehemu ya dili la kumnasa Diego Costa.
    Lakini inaeleweka wazi Mbelgiji huyo atakuwa mgumu kuridhishwa na kuhamia kwake Hispania kwa sababu kuhofia kunyanyaswa  ubaguzi wa rangi kufuatia adhabu laini iliyopewa Villarreal kwa udhalilishaji waliomfanyia Dani Alves wa Barcelona.
    Top target: Chelsea have begun talks with Atletico Madrid and Spain striker Diego Costa
    Costa ni chaguo namba moja la kocha Jose Mourinho katika usajili wa msimu ujao na boss huyo wa Chelsea anataka kumaliza biashara haraka iwezekanavyo kabla ya Kombe la Dunia.
    Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, anaetegemewa kuwemo kwenye kikosi cha Hispania kitakachoshiriki kombe la dunia, amefunga mabao 27 msimu huu lakini ana kipengele kinachomruhusu kuondoka kwa pauni milioni 32.
    Chelsea inaangalia kwanza mpango wa kupunguza gharama kwa kubadilishana ambapo Lukaku anatumiwa kama chambo.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.