Ndani: Luke Shaw ataenda kombe la dunia kwa nafasi ya Ashley Cole
Huduma yake: Cole aliichezea England katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Albania machi 2001.
ASHLEY Cole ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kuachwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya England kinachoenda kushirki kombe la dunia nchini Brazil kuanzia juni 12 hadi julai 13 mwaka huu.
Kocha wa England Roy Hodgson amempigia simu beki huyo mwenye miaka 33 na aliyeichezea timu ya taifa mechi 107 na kumueleza kuwa hatakuwepo katika kikosi chake na nafasi yake imechukuliwa na beki wa Southampton, Luke Shaw.
Cole ameandika kwenye mtandao wake wa Twita na kusema: "Nimepigiwa simu na Roy, tumekubaliana naye kuwa timu ya England itakuwa na vijana. Nadhani ni muda muafaka wa kustaafu kuchezea timu ya England sasa".
"Tuna kocha mkubwa na timu nzuri, nawatakia mafanikio mema. Nitawasapoti kama shabiki wa kweli. Namshukuru kila mtu aliyenipenda na ambaye hakunipenda, niamini, naumia sana kutolichezea taifa langu".

Hodgson anatarajia kutangaza kikosi cha timu ya Taifa ya England leo majira ya saa 8:00 mchana.
P
0 comments:
Post a Comment